Wahajiri haramu 170 raia wa Senegal waliokuwa
wamekusudia kuelea barani Ulaya na waliokuwa wamehifadhiwa katika kambi
maalumu mjini Tripol, Libya wamerejeshwa makwao.
Taarifa zaidi zinasema kuwa, wahajiri hao walirejeshwa
Alkhamisi ya jana katika fremu ya mpango wa kuwarejesha nyumbani
wahajiri, mpango ambao unasimamiwa na Shirika la Kimataifa la Wahajiri
(OIM). Kwa mujibu wa ripoti hiyo, karibu wahajiri wengine wapatao 200
raia wa Niger, walirejeshwa makwao siku ya Jumanne iliyopita kutoka
Libya ambako baada ya kutiwa mbaroni, waliwekwa katika kambi maalumu.
Mwaka jana Shirika la Kimataifa la Wahajiri (OIM) lilitangaza kuwa,
liliwasaidia wahajiri 1589 kurejeshwa makwao kwa hiari wakati walipokuwa
wakijaribu kuelekea barani Ulaya. Taarifa iliyotolewa mwezi Oktoba
mwaka jana na OIM ilisema kuwa, zaidi ya wahajiri elfu tano walikuwa
tayari wamefariki dunia tangu mwezi Aprili mwaka huo.
Njia kuu ambayo mara nyingi hutumiwa na wahajiri hao kuelekea barani
Ulaya wanakodhania kwamba wanaweza kupata maisha mazuri, ni Libya.
No comments:
Post a Comment