Mkuu wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya Federica
Mogherini aitahadharisha Marekani dhidi ya kuingilia shughuli za kisiasa
barani Ulaya baada ya maafisa wa Marekani kutaka kujuwa taifa gani
litajitowa baada ya Uingereza.
Mogherini amekaririwa akisema baada ya kukamilisha mikutano yake na
maafisa wa serikali ya Marekani akiwemo waziri wa mambo ya nje Rex
Tillerson kwamba "Hatuingilii siasa za Marekani na watu wa Ulaya
wanategemea Marekani haitoingilia siasa za Ulaya."
Mwaka jana
Trump alipongeza uamuzi wa Uingereza kujitowa Umoja wa Ulaya katika kura
ya maoni inayotajwa kama "Brexit" na kuzusha wasi wasi katika umoja huo
wote kwamba yumkini akataka kuyumbisha mradi wa muungano wa umoja huo
wa Ulaya.
Mogherini amesema "Naamini umoja wa Umoja wa Ulaya hivi leo unajidhihirisha zaidi kuliko ilivyokuwa miezi michache iliopita."
Amesema
Uingereza itaendelea kuwa nchi mwanachama wa Umoja wa Ulaya kwa angalau
kwa miaka mengine miwili na haitoweza kuzungumzia makubaliano yoyote
ya biashara peke yake na nchi yoyote ya tatu hadi hapo itakapokuwa
imeondoka Umoja wa Ulaya.
Kuhujumu Umoja wa Ulaya ni wenda wazimu
Aliyekuwa balozi wa Marekani kwa Umoja wa Ulaya Anthony Gardner.
Tokea
ushindi wake katika uchaguzi wa mwezi wa Novemba viongozi kadhaa wa
nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya wamemkosowa Trump kutokana na kauli
zake za kugawa watu huku Kansela Angela Merkel wa Ujerumani akisema
"Sisi nwananchi wa Ulaya hatima yetu iko mikononi mwetu."
Mogherini
amekutana na waziri wa mambo ya nje wa Marekani Tillerson pamoja na
maafisa wengine wa serikali ya Marekani mjini Washington.
Wakati
huo huo Mogherini ametaja kwamba Ikulu ya Marekani bado haikumchaguwa
balozi wa Marekani kwa Umoja wa Ulaya ambayo ina nchi wanachama 28
ambazo itabidi zimridhie katika utaratibu uliokuwa ukitumika kwa muda
mrefu.Wanasiasa wameelezea kutofurahishwa kwao juu ya uwezekano wa
kuteuliwa kwa Theodore Roosevelt Malloch kushika wadhifa huo.
Kabla
ya kuondoka kwenye wadhifa wake mwezi wa Januari balozi wa zamani wa
Marekani kwa Umoja wa Ulaya Anthony Gardner aliuonya utawala wa Trump
kutounga mkono kuvunjika kwa umoja huo.
Gardner aliyeteuliwa na
rais wa zamani wa Marekani Barack Obama amesema timu ya mpito ya Trump
imewasiliana na maafisa kadhaa wa Umoja wa Ulaya kabla ya kuapishwa kwa
Trump na kuwauliza nchi gani yumkini ikajitowa kwenye umoja huo baada ya
Uingereza.
Gardner amesema katika mkutano wake wa mwisho na
waandishi wa habari "kufikiri kuunga mkono kumegeuka kwa Ulaya
tutatukuwa tunaendeleza maslahi yetu utakuwa ni upuuzi mtupu.Ni wenda
wazimu".
Kauli za Trump zazusha mashaka
Mkuu
wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya Federica Mogherini akiwa na waziri
wa mambo ya nje wa Marekani Rex Tillerson mjini Washington.
Wakati
wa kampeni yake Trump aliapa kuutupilia mbali mkataba wa Iran iliofikia
na mataifa yenye nguvu duniani hapo mwaka 2015 na kudhibiti ipasavyo
mpango wa nyuklia wa nchi hiyo ili nchi hiyo iondolewe vikwazo vya
kiuchumi ilivyowekewa.
Suala la kunusurika kwa mkataba huo liko
wazi itategemea iwapo utawala wa Trump utajitowa kwenye makubaliano
hayo ya kimataifa. Hata hivyo mwanasiasa huyo mwandamizin wa Umoja wa
Ulaya amesema Ikulu ya Marekani imemhakikishia kwamba mkataba huo
utabakia kama ulivyo.
Mogherini amewaambia waandishi wa habari
hapo Ijumaa amehakikishiwa kwa kile alichokisikia katika mikutano hiyo
juu ya nia ya kuendelea kutekeleza kikamilifu makubaliano hayo.
Mogherini
amesema jukumu lake kubwa wakati wa ziara yake hiyo mjini Washington
ilikuwa ni kuhakikisha kwamba mkataba wa Iran unanusurika katika utawala
wa Trump.
No comments:
Post a Comment