Waziri wa zamani wa mambo ya nje Frank -Walter
Steinmeier amechaguliwa kuwa rais mpya wa Ujerumani Jumapili
(12.02.2017) wadhifa wa heshima ambao hauna madaraka makubwa ya
utendaji.
Mwanasiasa huyo mwenye umri wa miaka 61 ambaye mara kwa mara
uchunguzi wa maoni umekuwa ukimuonyesha kuwa ndie mwanasiasa mashuhuri
kabisa nchini ataliwakilisha taifa hilo lenye nguvu kubwa za kiuchumi
barani Ulaya nchi za nje na atatumika kama mtu mwenye kuheshimika na
kuaminika kwa taifa.
Wanachama wenzake wa chama cha Social
Demokrat (SPD) wanataraji kuchaguliwa kwake kutaimarisha nafasi yao
wakati mgombea wao Martin Schulz spika wa zamani wa bunge la Ulaya
akijitayarisha kupambana na Kansela Angela Merkel kuwania ukansela
katika uchaguzi uliopangwa kufanyika mwezi wa Septemba.
Apata kura 931
Frank-Walter Steinmeier akihutubia bungeni.
Steinmeier
amepata kura 931 kati ya 1,260 zilizopigwa baada ya mmugano wa
kihafhidhina wa Merkel kukosa mgombea wao wenyewe aliye imara kukubali
kumuunga mkono kuchukuwa nafasi ya Joachim Gauck mchungaji wa zamani
mwenye umri wa miaka 77 kutoka iliokuwa Ujerumani mashariki.
Kura
hiyo imepigwa katika bunge la Ujerumani mjini Berlin katika kikao
maalum cha bunge la shirikisho kilichowajumuisha wabunge wa taifa na
wawakilishi kutoka majimbo 16 ya Ujerumani wakiwemo wabunge na pia
wasanii,waandishi, wanamuziki na kocha wa timu ya soka ya taifa Joachim
Loew.
Steinmeier mmojawapo wa wanasiasa mashuhuri nchini
Ujerumani ametumika mara mbili kama waziri wa mambo ya nje chini ya
utawala wa Merkel kwa jumla ikiwa ni miaka saba.
Juu ya kwamba
mwanasheria huyo ni mtu muangalifu wakati akitowa hotuba zake wakati wa
kampeni ya mwaka jana ya urais wa Marekani alimwita Donald Trump kuwa
"mhubiri wa chuki"
Baada ya tajiri huyo kushinda uchaguzi
Sreinmeier amesema uhusiano utakuwa mgumu na kwamba wafanyakazi wake
walikuwa wakihangaika kupata ufasaha wa msimamo wa Trump katika sera
yake ya kigeni.Steinmeier atashika wadhifa huo Machi 19.
Gauck apongezwa
Rais anayeondoka madarakani Joachim Gauck akishangiliwa.
Spika
wa bunge la Ujerumani Norbert Lamert amewakaribisha wabunge 1,260
bungeni mjini Berlin kwa ajili ya kumchaguwa mtu wa kushika nafasi ya
Rais Joachim Goacja ambaye amejiuzulu kutokana na umri wake kuwa mkubwa.
Mwanzoni mwa kikao hicho cha bunge cha 16 kwa mara nyengine tena spika
huyo amempongeza rais huyo anayeondoka madarakani katika hotuba ya
kusisimuwa ambapo amesema "Mshikamano wa raia ulikuwa muhimu sana kwake"
Gauck pia amekuwa akisisitiza mara kwa mara jamii haipaswi kuhofu au
kugawika hata wakati huu wa vitisho vya magaidi.Gauck alieonekana
kuguswa na wabunge na wawawakilishi wengine wa majimbo waliokuwa
wakimshangalia ukumbini.
Frank - Walter Steinmeir wa chama cha
Social Demokratic anataka kupambana na kuongezeka kwa hali ya wasi wasi
katika jamii wakati atakaposhika wadhifa huo wa juu wa
taifa.Akizungumza katika mapokezi ya chama chake katika bunge hilo la
shirikisho amesema "Ningelipenda kusema kwamba changamoto ni kubwa
kwamba hatuwezi kuendelea nayo migogoro na mizozo inayotuzunguka."
Kuchaguliwa kwake kulikuwa na uhakika
Frank -Walter Steinmeier akipiga kura yake.
Mwenyekiti
wa chama cha SPD Sigmar Gabriel amevishukuru vyama vyengine waliounga
mkono ugombea wa Steinmeier katika wadhifa huo jambo ambalo halijitokezi
katika mwaka wa uchaguzi.Katika mkutano maalum wa chama cha SPD wa
bunge ametangaza uteuzi huo wa Steinmeier kwa wadhifa huo ni zawadi ya
kumuaga ya chama chake.
Tokea mwanzo kuchaguliwa kwa Steinmeier
kwenye wadhifa huo kulikuwa ni jambo la uhakika: waziri huyo wa mambo
ya nje wa zamani alikuwa akiungwa mkono na mmungano wa kihafidhina wa
vyama ndugu vya CDU na CSU ambavyo vina wingi wa viti bungeni.
Chama
cha sera kali za mrengo wa kushoto Die Linke,chama cha sera kali za
mrengo wa kulia Chama Mbadala kwa Ujerumani AfD na kile cha Pirate
vilikuwa na wagombea wao lakini havikuwa na nafasi kabisa ya kushinda.
No comments:
Post a Comment