Kenya imeanzisha mkakati wa huduma za 'Halal' za kitalii kwa ajli ya ongezeko la watalii Waislamu nchini humo.
Kwa mujibu wa Shirika la Habari la IQNA, Halmashauri ya
Kuratibu Utalii nchini Kenya TRA imesema imeandaa sheria za kutoa vibali
vya 'Halal' kwa ajili ya maeneo ya kitalii yanayolenga kuwahudumia
watalii Waislamu wanaotaka huduma kwa msingi wa mafundisho ya Kiislamu.
Wakuu wa utalli nchini Kenya wanasema, idadi ya watalii Waislamu
wanaofika nchini Kenya inazidi kuongoezeka. Kwa mfano mwaka 2015, Kenya
ilipokea watalii 40,874 kutoka Umoja wa Falme za Kiarabu, UAE, katika
hali ambayo idadi hiyo ilikuwa 24,828 mwaka 2014.
Mkurugenzi Mkuu wa TRA Lagat Kipkorir amesema viwango vya utalii
Halal vinatayarishwa kwa ushuhirikiano na Idara ya Viwango Kenya.
"Tumetayarisha mpango wa kina kutunga kanuni, kuwashirikisha washikadau,
kudhamini viwango, na mafunzo kabla ya kuzindua rasmi utalii Halal,"
amesema Kipkorir.
Kwa ujumla maeneo yanayotoa huduma za kitalii ya Waislamu kwa kawaida
huwa hayana pombe, kuna sehemu tafauti za kuogolea wanaume na wanawake
na mfumo mzima wa upishi huzingatia kikamilifu chakula halali.
Kenya inahesabiwa kama mojawapo ya nchi muhimu zaidi za kitalii
barani Afrika na kila mwaka idadi kubwa ya watalii kutoka kote duniani
huitembelea nchi hiyo.
No comments:
Post a Comment