Mkuu wa kituo cha utafiti wa kistratijia cha
Halmashauri ya Kuainisha Maslahi ya Mfumo wa Iran amevielezea vitisho
ilivyotoa Marekani kufuatia jaribio la kombora lililofanywa na Iran kuwa
ni "makeke hewa".
Akizungumzia
kauli za vitisho zilizotolewa na serikali ya Marekani, Ali Akbar
Veleyati amesema, hii si mara ya kwanza kwa mtu asiye na tajiriba kutoka
Marekani kutoa vitisho dhidi ya Iran. Amefafanua kuwa baada ya muda
kupita, Trump ataelewa kwamba utoaji kauli hewa za majigambo na makeke
dhidi ya Iran kutazidi kushusha hadhi na itibari yake tu mbele ya fikra
za walimwengu.
Dakta
Velayati, ambaye pia ni mshauri wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya
Kiislamu katika masuala ya kimataifa amesisitiza kwa kusema: "Ni vizuri
huyu bwana (Trump) au watu wengine ambao ndio kwanza wamepata tajiriba
ya kuongoza serikali, wakajifunza kutokana na uzoefu wa wale walioongoza
serikali nchini Marekani huko nyuma ili kuelewa kwamba wasifanye makeke
yasiyo na msukumo na kujifanya kinyago mbele ya nchi nyingine na fikra
za walimwengu".
Mkuu wa kituo cha utafiti wa kistratijia cha Halmashauri ya Kuainisha
Maslahi ya Mfumo wa Iran ametoa jibu hilo, baada ya kama ilivyokuwa
huko nyuma, viongozi wa serikali ya Marekani kutoa kauli za vitisho
dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu kwa sababu ya jaribio ililofanya hivi
karibuni la kombora la balistiki.
Rais
Donald Trump wa Marekani aliandika katika ukurasa wake wa kijamii wa
Twitter hapo jana kuwa, Iran imepewa onyo kwa sababu ya jaribio
ililofanya la kombora la balistiki.
Hii ni
katika hali ambayo Waziri wa Ulinzi wa Iran Brigedia Jenerali Hussein
Dehqan alithibitisha siku ya Jumatano kuhusu kufanyiwa jaribio kombora
hilo na kusisitiza kwamba Tehran haitoruhusu ajinabi yeyote kuingilia
masuala yake ya kiulinzi…/
No comments:
Post a Comment