Ghasia na machafuko yameendelea kuukumba mji
mkuu wa Ufaransa, Paris kwa siku kadhaa baada ya kuenea ripoti kuwa
maafisa wa polisi ya nchi hiyo wamempiga vibaya na baadaye kumnajisi kwa
kijiti mwanaume mwenye asili ya Afrika katika viunga vya mji wa Paris.
Walalamikaji wamechoma moto shule ya chekechea, magari na mapipa ya jalala na kuvunja viyoo vya nyumba za eneo hilo.
Ripoti zinasema waandamanaji waliokuwa wanejifunga vitambaa usoni waliharibu na kuchoma moto madazeni ya magari ya watu binafsi.
Hadi
kufikia jana ghasia na machafuko hayo yalikuwa yameenea katika
vitongoji kadhaa vya Paris karibu na eneo la Aulnay-sous-Bois ambako
inasemekana maafisa wa polisi ya Ufaransa alimpiga na kumnajisi kijana
huyo mwenye umri wa miaka 22 aliyetajwa kwa jina moja tu la Theo hapo
tahere 2 mwezi huu wa Februari.
Kijana huyo ambaye amejeruhiwa vibaya amelazwa hospitalini ambako amefanyiwa upasuaji.
Ukatili na unyama huo wa polisi ya Ufaransa umesababisha maandamano
na machafuko kwa usiku kadhaa sasa kaskazini mwa Paris na viunga vyake.
Waandamanaji mbali na kulaani vikali ukatili wa polisi na namna
wanavyotumia vibaya mamlaka yao, wametaka uadilifu utendeke.
Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ufaransa, Bruno Le Roux amesema maafisa hao wanne wa polisi wamefunguliwa mashtaka ya kufanya mashambulizi makali na kunajisi.
No comments:
Post a Comment