Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Thursday, February 9, 2017

UN: ZAIDI YA WAISLAMU 1000 WAMEUAWA KATIKA OPERESHENI ZA JESHI LA MYANMAR

Maafisa wawili wa ngazi ya juu wa Umoja wa Mataifa wamesema kuwa, zaidi ya Waislamu 1000 wa kabila la Rohingya wameuawa katika operesheni za jeshi la Myanmar kaskazini mwa nchi hiyo.
Maafisa hao wa UN ambao wanafuatilia wimbi la Waislamu wanaokimbia kutokana na ukatili unaoendelea dhidi yao nchini Myanmar wamesema kuwa, takwimu za uharibifu unaotokana na operesheni za jeshi la nchi hiyo, ni zaidi ya kiwango kilichotajwa awali na serikali hiyo. Hii ni katika hali ambayo viongozi wa serikali wamedai kuwa, tangu kulipotekelezwa operesheni hizo katika mkoa wa Rakhine mwaka jana, watu wasiofikia 100 ndio waliouawa.
Jamii ya Waislamu katika tabu nchini Myanmar
Ofisi ya Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya Haki za Binaadamu, sanjari na kutoa ripoti inayohusiana na ukatili wa kutisha wa askari wa Myanmar dhidi ya Waislamu imesema kuwa, askari hao walihusika na mauaji dhidi ya watoto wachanga, watoto wadogo, wanawake, wazee pamoja na kuwanajisi wanawake. Kabla ya hapo serikali ya Myanmar ilikadhibisha tuhuma hizo na kutaka ufanyike uchunguzi kuhusiana na suala hilo. Hata hivyo maafisa wa serikali hawakuziruhusu timu za uchunguzi kufika eneo la tukio kwa khofu ya kufichuliwa ukatili huo.
Wanawake Waislamu nchini Myanmar wanaofanyiwa ukatili wa kutisha na Mabudha
Wakati huo huo Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani amelaani jinai wanazofanyiwa Waislamu wa kabila la Rohingya nchini Myanmar. Papa Francis, kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani ameyasema hayo jana na kuongeza kuwa, Waislamu wa Myanmar wananyanyaswa kwa miaka mingi sasa na wanauawa na kuteswa kinyama kwa sababu tu ya kutaka waishi kwa mujibu wa utamaduni na mafundisho ya dini yao. 

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages