Ligi ya Mabingwa barani Ulaya inarejea huku kukiwa na
mechi kadhaa za kusisimua hasa katika mechi za kwanza nne za mkondo kwa
kwanza wa hatua ya 16 za mwisho
Jumanne, Barcelona watakuwa mjini Paris kupambana na PSG ikiwa ni kwa
mara ya tatu katika misimu minne katika hatua ya mwondowano. Barca
walishinda katika robo fainali za 2013 na 2015 na wakashinda taji msimu
huo. Pia utawaleta pamoja washambuliaji wa Uruguay, ambapo Edison Cavani
wa PSG atakutana na Luis Suarez
Benfica na Borussia Dortmund,
wote wakiwa mabingwa wa zamani, wanakutana katika mtanange ambao timu
zote zinaonekana kuwa zenye uwezo sawa. Dortmund walikuwa wakali sana
katika hatua ya makundi ambapo walimaliza katika nafasi ya kwanza mbele
ya Real. Hata hivyo BVB hawajawa imara sana katika ligi ya nyumbani
wakati Benfica wamepoteza mara mbili tu katika mechi zake 20 za nyumbani
dhidi ya wapinzani wa Ujerumani.
Siku ya Jumatano, mjini Munich,
Arsenal watajaribu kutafuta ushindi dhidi ya adui wanayemfahamu vizuri
sana, Bayern. Timu hizo zinakutana kwa mara ya nne katika misimu mitano
huku The Gunners wakitumai kuepuka kubanduliwa nje katika hatua hii kwa
mwaka wa saba mfululizo. Viwili kati ya vichapo hivyo vilikuwa mikononi
mwa Bayern mwaka wa 2013 na 2014
Real Madrid wana mtihani mkali
dhidi ya Napoli, ambao hawajashindwa katika mechi 18, wakati wakilenga
kuwa timu ya kwanza kuhifadhi kombe la Ligi ya Mabingwa. Aliyekuwa nyota
wa Argentina Diego Maradona anatarajiwa kujiunga na mashabiki 10,000 wa
Napoli watakaomiminika katika uwanja wa Santiago Bernabeu. Maradona
alikuwa nahodha wa Napoli
Michuano minne ya mkondo wa kwanza itachezwa wiki ijayo, wakati ya marudiano ikichezwa Machi 7/8 na 14/15
No comments:
Post a Comment