Takribani watu 18 wameuwawa baada ya gari ilililokuwa na viripuzi
kuripuka karibu na eneo lenye pirikaprika nyingi mjini Mogadishu,
Somalia. Afisa mwandamizi katika eneo la tukio Mohamed Jilibey
alithibitisha kuhesabu maiti za idadi hiyo ya watu na kuongeza kuwa watu
wengine zaidi ya 25 wamejeruhiwa. Mripuko huo unahesabiwa kuwa wa
kwanza mkubwa kutokea katika mji mkuu wa Somalia tangu kufanyika
uchaguzi uliomwingiza madarakani rais Mohamed Abdullahi Mohamed
anayetambulika pia kwa jina la Farmajo. Shambulio hilo linaziweka wazi
changamoto anazokabiliana nazo rais huyo mpya, ambae amerithi utawala
wenye udhibiti mchache wa ardhi ya Somalia kutokana na uwepo wa kundi la
al Shabaab. Majeshi ya Umoja wa Afrika yalifanikiwa kuliondosha kundi
hilo katika viunga vya jiji la Mogadishu August 2011 lakini wanamgambo
wake wameendelea kuyadhibiti maeneo ya vijijini na kurejea mara kwa mara
kufanya mashambulizi katika maeneo ya mji huo mkuu wa Somalia.
Post Top Ad
Your Ad Spot
Sunday, February 19, 2017
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
Author Details
Ut wisi enim ad minim veniam, quis nostrud exerci tation ullamcorper suscipit lobortis nisl ut aliquip ex ea commodo consequat. Duis autem vel eum iriure dolor in hendrerit in vulputate velit esse molestie consequat.
No comments:
Post a Comment