Watu wasiopungua 39 wameuawa leo Jumapili
wakati gari lililokuwa limesheheni mabomu liliporipuka katika makutano
ya barabara katika mji mkuu wa Somalia, Mogadishu.
Mlipuko
huo ni hujuma ya kwanza kubwa kujiri Somalia tokea aingie madarakani
rais mpya wa Somalia Mohammad Abdullahi Mohamad, maarufu kama
Farmaajo, wiki jana.
Walioshuhudia
wanasema mlipuko huo ulilenga makutano ya barabara katika mtaa wa
Madina, kusini mwa Mogadishu. Mlipuko huo ulilenga wanajeshi na
wafanyabiashara pamoja na wapita njia katika eneo hilo lenye msongamano
mkubwa wa watu na magari. Baadhi ya walioshuhudia wanasema idadi
iliyotangazwa ni chini ya wale waliouawa katika hujuma hiyo ya kigaidi.
Shambulizi hilo linaashiria changamoto alizonazo rais mpya wa Somalia
ambaye amerithi serikali ambayo haikuwa na udhibiti katika maeneo mengi
ya nchi hiyo ambayo yanakaliwa kwa mabavu na kundi la kigaidi la Al
Shabab.
Wanajeshi
wa kulinda amani wa Umoja wa Afrika Somalia AMISOM waliwatimua magaidi
wa Al Shabab kutoka Mogadishu Agosti mwaka 2011 lakini magaidi hao
wanaendelea kushikilia maeneo mengine ya nchi hiyo na hujipenyeza mara
kwa mara katika mji mkuu kutekeleza mashambulizi.
No comments:
Post a Comment