Uchunguzi mpya wa maoni Ujerumani unaonyesha chama
(SPD) kinaweza kuunda serikali ya mseto kwa kushirikiana na chama cha
Mazingira na kile cha mrengo wa kushoto Di Linke iwapo uchaguzi
utafanyika hivi karibuni Ujerumani.
Gazeti la "Bild am Sonntag" limeripoti Jumapili kwamba kwa mujibu wa
uchunguzi wa maoni Chama hicho cha SPD kimeupiku tena muungano wa
wahafidhina wa chama cha Angela Merkel cha Christian Demokrat(CDU) na
chama ndugu cha Christian Social Union (CSU).
"Sonntagstrend"
uchunguzi wa maoni uliofanywa na asasi ya kuchunguza maoni ya Emnid
umeonyesha chama cha SPD kikiimarika kwa asilimia moja katika kipindi
cha wiki moja kufikia asilimia 33 wakati chama cha CDU na chama ndugu
cha jimbo la Bavaria CSU vikishuka kwa asilimia moja na kuwa katika
kiwango cha asilimia thelathini na mbili.
Matokeo hayo
yanaonyesha kwa mara ya kwanza katika baada ya kipindi cha miaka kumi
chama hicho cha mrengo wa wastani kushoto SPD kimevipiku vyama hivyo vya
kihafidhina katika uchunguzi wa maoni wa "Sonntagstrend" ambao asasi ya
Emnid imekuwa ikiufanya kila wiki kwa ajili ya gazeti la "Bild a
Sonntag".
Uchunguzi mwengine wa maoni wa hivi karibuni uliofanywa
kwa ajili ya gazeti la "Bild"na asasi ya Insa pia umeonyesha chama
hicho cha SPD kikiwa mbele ya kundi la vyama vya CDU/CSU kwa mara ya
kwanza baada ya kipindi cha muongo mmoja.
Nyekundu-nyekundu-kijani
Kansela Angela Merkel wa Ujerumani na kiongozi wa chama cha SPD Martin Schulz.
Wakati
vyama vya "Die Linke " cha sera kali za mrengo wa kushoto na kile cha
Mazingira vikiendelea kushikilia asilimia zao nane na saba kila mmoja
uchunguzi huo wa maoni unadokeza kwamba muungano wa serikali ya mseto wa
vyama vitatu vya mrengo wa kushoto ambao ungeitwa muugano wa rangi
nyekundu-nyekundu -kijani kwa mujibu wa mfumo wa rangi za kisiasa nchini
Ujerumani utakuwa na serikali ya viti vingi bungeni iwapo uchaguzi
utafanyika katika kipindi cha wiki moja inayokuja.
Mafanikio hayo
ya hivi karibuni ya chama cha SPD katika uchunguzi wa maoni umechangiwa
kwa kiasi kikubwa na kuchaguliwa kwa spika wa zamani wa bunge la Ulaya
Martin Schulz mwenye kipaji kuwa kiongozi wao kuchukuwa nafasi ya Sigmar
Gabriel ambaye amejiuzulu kama kiongozi wa chama ili kuwa waziri wa
mambo ya nje wa Ujerumani.
Chama rafiki kwa biashara cha Free
Demokratik (FDP) pia kimeendelea kushikilia umashuhuri wake kwa mujibu
wa uchunguzi huo wa maoni kwa kujipatia asilimia sita. Lakini chama
kinachopinga uhamiaji na chenye mashaka na Umoja wa Ulaya
kinachojulikana kama Chama Mbadala kwa Ujerumani (Afd) kimeendelea
kuporomoka kwa kupoteza asilimia moja na kufikia ailimia tisa kiwango
cha chini kabisa cha umashuhuri wake katika uchunguzi wa maoni katika
kipindi cha mwaka mmoja.
No comments:
Post a Comment