Dikteta aliyepinduliwa madarakani huko Misri amesisitiza kuwa visiwa vya Tiran na Sanafir ni milki ya nchi hiyo.
Hosni Mubarak Rais wa zamani wa Misri aliyepinduliwa madarakani
amesisitiza katika ujumbe wa sauti akiwahutubu wananchi katika
kumbukumbu ya kutimia mwaka wa sita tangu apinduliwe madarakani nchini
humo kuwa kwa mujibu wa hukumu iliyotolewa na mahakama ya nchi hiyo
visiwa viwili vya Tiran na Sanafir ni mali ya Misri. Saudi Arabia na
Misri zinahitilafiana kuhusu umiliki wa visiwa hivyo viwili vilivyopo
kaskazini mwa bahari Nyekundu.
Itakumbukwa kuwa Cairo mwaka iliafiki kuipatia Saudi Arabia visiwa
hivyo viwili kufuatika makubaliano yaliyofikiwa kati ya nchi mbili hizo;
na mkabala na hatua hiyo; Wasaudia pia wanapaswa kuwekeza katika uchumi
wa Misri, hata hivyo mapatano hayo yalibatilishwa na mahakama ya
Misri. Wananchi wa Misri wamekuwa wakiandamana pakubwa katika mji mkuu
Cairo na katika maeneo mengine ya nchi kulalamikia hatua hiyo ya
serikali ya kuipatia Saudia visiwa vyao. Watu zaidi ya 200 wametiwa
mbaroni na wengine kadhaa kuhukumiwa vifungo jela kwa kosa la kushiriki
katika maandamano hayo.
No comments:
Post a Comment