Sunday, February 19, 2017

PAPA AHIMIZA AMANI CONGO

Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Francis amewataka viongozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kuchukua hatua za haraka kutatua mgogoro wa kisiasa na kudhibiti machafuko pamoja na kulaani hasa matumizi ya watoto jeshini. Katika miezi ya hivi karibuni vurugu zimetapakaa katika maeneo tofauti ya taifa hilo, ikihusisha makabiliano yaliosababisha mauwaji katika eneo la Kasai, wakati huu ambapo Rais Joseph Kabila wa taia hilo hakuonyesha ishara ya kun'gatuka juu ya kwamba muda wake wa kuweko madarakani umemalizika Desemba. Ijumaa kulisambazwa picha zinazoonesha wanajeshi wa Congo wakiwauwa raia wasio na silaha katika maeno ya Kasai, wakati jana wapiganaji wa Kabila la Nande waliwauwa raia 25 katika eneo lenye vurugu la mashariki mwa taifa hilo ambapo vifo vingi viesababishwa kwa kutumia mapanga.

No comments:

Post a Comment