Naibu Waziri Mkuu wa Russia katika masuala ya
ulinzi amesema kuwa, Moscow inatengeneza makombora ambayo yana uwezo wa
kupenya kirahisi ngome za kujilinda na makombora za Marekani na kupiga
kulikokusudiwa.
Shirika la habari la IRNA
limemnukuu Dmitry Rogozin akisema hayo jana usiku na kuongeza kuwa,
makombora ya Russia yana uwezo wa kukwepa ngao za kujilinda na makombora
za Marekani zilizopo hivi sasa na zitakazokuja.
Amesema, ngao za kujilinda na makombora za Marekani hazina hatari yoyote hivi sasa kwa Russia zaidi ya kufanya uchokozi tu.
Itakumbukwa kuwa, tangu miaka mitatu
iliyopita, Marekani ilianza kuweka ngao zake za kujilinda na makombora
katika nchi za Ulaya Mashariki kwa madai ya kukabiliana na tishio la
makombora ya Russia na imeweka miundombinu za ngao zake hizo katika nchi
za Romania na Poland.
Kitendo cha Marekani cha kuweka ngao zake za kujilinda kwa makombora huko Ulaya Mashariki kimewakasirisha viongozi wa Russia.
Moscow imetangaza kuwa, hatua hiyo ya Marekani ni tishio la wazi kwa usalama wa kiistratijia wa Russia.
No comments:
Post a Comment