Waziri wa Mambo ya Ndani wa Jamhuri ya Afrika
ya Kati ametangaza habari ya kuendelea operesheni kadhaa za kupambana
na makundi yenye silaha.
Mtandao wa habari wa Africa Time
umemnukuu Jean-Serge Bokassa akitangaza habari hiyo na kusema kuwa,
suala la kurejesha utulivu katika nchi hiyo iliyokumbwa na machafuko
makubwa ni zito sana, hata hivyo serikali yake imeamua kupambana na
makundi ya waasi hususan katika eneo linalojulikana kwa jina la PK5.
Waziri wa Mambo ya Ndani wa Jamhuri ya
Afrika ya Kati amesema, eneo hilo lenye Waislamu wengi, wiki zilizopita
limeshuhudia mashambulizi ya watu wenye silaha walioua raia bila ya
hatia.
Wakati huo huo mwandadiplomasia mmoja wa
Jamhuri ya Afrika ya Kati amegusia machafuko yaliyoikumba nchi hiyo na
kusema kuwa, hali hiyo haiuhusu mji mkuu Bangui, pekee, bali iko katika
maeneo yote ya Jamhuri ya Afrika ya Kati kiasi kwamba wananchi wamekosa
imani na serikali.
Baadhi ya wakati zoezi la kuwapokonya
silaha waasi limepelekea makundi ya wanamgambo kufanya mashambulizi
katika maeneo mengine ya nchi hiyo yakiwemo ya mashariki.
Wimbi la mapigano limeongezeka kwenye
miezi ya hivi karibuni na kupelekea raia wengi wa Jamhuri ya Afrika ya
Kati kukimbia maeneo yao.
Itakumbukwa kuwa, Faustin-Archange
Touadéra alichaguliwa kuwa rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati mwezi Machi
2016, hata hivyo hadi leo hii serikali yake imeshindwa kurejesha amani
na utulivu nchini humo.
No comments:
Post a Comment