Saturday, February 11, 2017

MAREKANI YAPINGA UTEUZI WA FAYYAD KWENYE UMOJA WA MATAIFA

Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Antonio Guterres ameutetea uamuzi wake wa kumteua waziri mkuu wa zamani wa mamlaka ya Palestina Salam Fayyad kuwa mjumbe wa Umoja huo wa kuushughulikia mgogoro wa nchini Libya. Uteuzi huo hauungwi mkono na Marekani. Hata hivyo msemaji wa Umoja wa Mataifa ameeleza kwamba uamuzi huo umetokana na uwezo wa bwana Fayyad wa kuifanya kazi hiyo. Lakini balozi wa Marekani kwenye Umoja wa Mataifa Nikki Haley amesema nchi yake haiungi mkono kwa sababu kwa muda mrefu Umoja wa Mataifa umekuwa unaibagua Israel. Guterres anatafuta kuungwa mkono na wanachama wote15 ili kukamilisha uteuzi wake. Ufaransa na Sweden zinaunga mkono uteuzi wa Fayyad, afisa wa zamani wa benki ya dunia anayejulikana kwa rekodi yake ya kupambana na ufisadi.

No comments:

Post a Comment