Mchezaji
wa Marekani wa mchezo wa fencing mwenye Imani ya dini ya Kiislamu,
Ibtihaj Muhammad amejikutana akizuiliwa kwa masaa mawili katika kiwanja
cha ndege bila kuambiwa sababu ya kuzuiliwa kwake na hata yeye mwenyewe
akiwa hajui sababu ya wafanyakazi wa kiwanja hicho kumzuia.Akielezea
tukio hilo, alisema amekuwa akisikia tu watu wakiongea kuwa kuna nchi
saba zimezuiliwa kuingia Marekani lakini hakuwa akijua zaidi na lakini
na yeye imemtokea na anahisi wafanyakazi wa uwanja wa ndege aliotumia
walidhani na yeye ni mmoja wa wakimbizi kutoka mataifa yaliyozuiliwa
lakini anashangaa kwanini alizuiliwa na hali yakuwa anakila kitu
kinachomtambulisha kuwa Mmarekani.
“Wiki
kadhaa zilizopita nilizuiliwa na wafanyakazi wa uwanja wa ndege kwa
masaa mawili, sijui kwanini. Siwezi kusema kwanini ilinitokea, lakini
najua mimi ni Mwislamu na nina jina la Kiarabu, na hata hivyo
naiwakilisha timu ya Marekani na nina vifaa vya Olympic lakini hilo bado
halijabadili mwonekano wangu na jinsi watu wanavyonichukulia,” alisema
Muhammad.
Kuziliwa
kwa Ibtihaj Muhammad kumekuja ikiwa ni sehemu ya agizo la Rais wa
Marekani, Donald Trump kuzuia wakimbizi kutoka mataifa saba yenye imani
kali ya Kiislamu mpaka watakapoimarisha hali ya usalama na kuwa imara
ndipo wataruhusiwa tena kuendelea kuingia nchini humo.
Ibtihaj
Muhammad ni Mmarekani wa kwanza mwenye imani ya Kiislamu kushinda medali
katika mashindano ya Olimpiki akiwa amevaa hijabu mwanzo mpaka mwisho
wa mashindano.
No comments:
Post a Comment