Saturday, February 11, 2017

TAARIFA YA HABARI ZA ULIMWENGU KUTOKA IDHAA YA KISWAHILI YA DW

Marekani imezuia uteuzi wa aliyekuwa Waziri Mkuu, wa Wapalestina Salam Fayyad kuwa mjumbe mpya wa Umoja wa Mataifa kwa Libya. Balozi wa Marekani Nikki Haley amesema kupitia taarifa kuwa hakuunga mkono ishara ambayo uteuzi huo ungesababisha katika Umoja wa Mataifa ambako taifa la Palestina halina uanachama kamili. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres alikuwa amelifahamisha baraza la Usalama nia yake ya kumtaja Fayyad kuongoza Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Libya na asaidie kusimamia mazungumzo ya amani kuhusu makubaliano ya kisiasa yananayoyumba. Haley amesema Marekani imevunjika moyo kuona barua kutoka kwa Guterres, huo ukiwa uteuzi wake wa kwanza wa mjumbe katika eneo linalokabiliwa na vurugu kubwa. Wapalestina wameshutumu vikali hatua hiyo ya Marekani na kuitaja kuwa ni ubaguzi wa hadharani. Fajad aliye na umri wa miaka 64 alikuwa Waziri Mkuu wa Mamlaka ya Wapalestina kwanzia mwaka 2007 hadi 2013
Taarifa ya Habari za Ulimwengu kutoka Idhaa ya Kiswahili ya DW

No comments:

Post a Comment