Merkel asisitiza juu ya kuukabili ugaidi
Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amesema hatari kama ile
inayotokana na magaidi wanaojiita Dola la Kiislamu IS au Boko Haram
haiwezi kuzuiwa na nchi moja peke yake, na kwa hivyo ametoa mwito wa
kujengwa mfumo wa pamoja duniani ili kuikabili hatari hiyo. Akiwa kwenye
mkutano wa kimataifa kuhusu usalama unaofanyika mjini Munich, Merkel
ameahidi kwamba Ujerumani itajitahidi kulifikia lengo la kuchangia
asilimia mbili ya pato jumla la nchi yake kwa ajili ya bajeti ya ulinzi
ya jumuiya hiyo. Makamu wa rais wa Marekani Mike Pence katika hotuba
yake aliwahakikishia washirika wa barani Ulaya kwamba Marekani
itaendelea kusimama nao kwa uthabiti katika jumuiya ya NATO. Hata hivyo
Pence amezitaka nchi wanachama wa jumuiya hiyo zitoe mchango wao kwa
haki. Pence amesema wakati sasa umefika wa kuchukua hatua zaidi ili
kupambana na changamoto mbalimbali za kijeshi zilizopo duniani.
No comments:
Post a Comment