Wafungwa 17 wameuawa kwa kupigwa risasi na
askari gereza walipokuwa katika harakati za kutoroka jela huko Papua New
Guinea, nchi ndogo iliyoko kusini magharibi mwa bahari ya Pacific.
Ingawaje tukio hilo lilitokea Ijumaa iliyopita, lakini habari
zake zimewekwa wazi na vyombo vya dola na waandishi wa habari Jumatatu
hii.
Anthony Wagambie, Kamanda Mkuu wa Polisi eneo la Lae amethibitisha
kutokea tukio hilo huku akiwatahadharisha wananchi kuwa macho, kwani
makumi ya wafungwa hao walifanikiwa kutoroka na ni hatari kwa usalama.
Habari zinasema kuwa, tukio hilo lilifanyika katika gereza la Buimo
mjini Lae, ambapo mbali na wafungwa 17 kuuawa kwa kufyatuliwa risasi,
wengine zaidi ya 50 walifanikiwa kutoweka.
Mwaka jana, tukio kama hilo lilifanyika nchini humo, ambapo wafungwa
12 waliuawa, 18 kujeruhiwa huku 94 wakifanikiwa kutoroka jela.
Kituo cha Kurekebisha Tabia cha Buimo chenye uwezo wa kubeba wafungwa 400, kwa sasa kimefurika wafungwa zaidi ya 1000.
No comments:
Post a Comment