Gari lililokuwa limetegwa bomu limeripuka
katika kitongoji kimoja kusini mwa Baghdad mji mkuu wa Iraq na kuuwa
makumi ya watu na kujeruhi wengine wengi.
Mlipuko
huo umetokea leo wakati gari moja ambalo lilikuwa limetegwa mada mabomu
liliporipuka katika mtaa mmoja wenye gereji nyingi za wauza magari huko
katika wilaya ya Hayy al Shurta mjini Baghdad.
Ripoti
zinasema kuwa, watu 51 wameuawa katika mlipuko huo na wengine kadhaa
wamejeruhiwa. Mlipuko huo wa leo umetokea siku moja baada ya ule wa
jana katika kitongoji cha Sadr mjini Baghdad na kuua watu wasiopungua
15. Raia wengine 50 walijeruhiwa.
Vyombo vya habari vya Iraq vimeripoti kuwa, kundi la kigaidi la Daesh limetangaza kuhusika na mlipuko huo.
Kundi la Daesh limezidisha mashambulizi ya kigaidi katika maeneo
mbalimbali ya Iraq katika kulipiza kisasi kipigo kikali kutoka jeshi la
Iraq hususan katika mji wa Mosul kaskazini mwa nchi hiyo.
No comments:
Post a Comment