Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Friday, February 17, 2017

IRAN YALAANI MAUAJI YA WATU 80 KATIKA HARAM YA SUFI NCHINI NCHINI PAKISTAN


Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imelaani shambulio la kigaidi lililotokea jana Alkhamisi katika mkoa wa Sindh nchini Pakistan, ambapo makumi ya watu waliuawa na wengine wengi kujeruhiwa.
Bahram Qassemi, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Iran sanjari na kutoa mkono wa pole kwa serikali ya Pakistan, waathirika wa hujuma hiyo ya kigaidi na taifa kwa ujumla, amelitaja shambulizi hilo kama 'jinai mbaya ya kutisha'.
Qassemi amesema mbinu chafu kabisa ya kisiasa ni kutumia ugaidi na vitisho kwa maslahi ya kisiasa akisisitiza kuwa, juhudi za pamoja na za dhati zinahitajika ili kung'oa mizizi ya ugaidi katika eneo na kote duniani. 
Wahanga wa hujuma ya Alkhamisi mkoani Sindh 
Zaidi ya watu 80 wakiwemo watoto wadogo 20 waliuawa na wengine 250 kujeruhiwa jana Alkhamisi, baada ya magaidi wa Daesh kushambulia kwa bomu Haram ya Kisufi ya Hazrat Lal Shahbaz Qalandar, katika mji wa Sehwan Sharif, mkoani Sindh.
Magaidi wapatao 39 wa kundi la kitakfiri la Daesh/ISIS wameuawa na maafisa usalama kufuatia hujuma hiyo, baadhi wakiuawa kwa kufyatuliwa risasi mkoani Sindh, na wengine katika eneo la Khyber Pakhtunkhwa.  
Septemba mwaka jana, watu zaidi ya 23 waliuawa na makumi ya wengine kujeruhiwa katika shambulio jingine la kigaidi lililofanywa ndani ya msikiti katika Sala ya Ijumaa wilayani Mohmand nchini Pakistan.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages