Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Tuesday, February 7, 2017

SAUDIA KATIKA MSHTUKO, WAHKA BAADA YA MJII MKUU RIYADH KULENGWA KWA KOMBORA LA YEMEN

Hatua ya Jeshi la Yemen ya kuvurumisha kwa mara ya kwanza kombora la balistiki katika kituo cha kijeshi katika mji mkuu wa Saudia Arabia, Riyadh ni jambo ambalo limeibua mshtuko mkubwa katika ukoo wa Aal Saud unaotawala ufalme huo.
Usiku wa kuamkia Jumatatu ya jana, kombora la kisasa la balistiki la Jeshi la Yemen lililenga kituo cha kijeshi katika eneo la al-Mazahamiah mjini Riyadh. Shambulizi hilo la kwanza la aina yake limeibua mshtuko, hofu na wahka katika Ufalme wa Saudia. Kwa mujibu wa tovuti ya Al-Najmul Thaqib, Mwanamfalme Mohammad bin Salman, Naibu Mrithi wa Kiti cha Ufalme na Waziri wa Vita wa Saudia ameitisha kikao cha dharura na rais aliyejizulu wa Yemen Abdu Rabuh Mansour Hadi kufuatia hujuma hiyo iliyolenga Riyadh.
Ni karibu miaka miwili sasa tokea Saudia inazishe hujuma ya kidhalimu dhidi ya Yemen ambapo karibu Wayemen 12,000 wameuawa na makumi ya maelfu ya wengine kujeruhiwa. Hivi sasa inaelekea kuwa mlingano wa vita vya Yemen unabadilika na moja ya ishara hizi ni  hujuma hiyo ya Jeshi la Yemen dhidi ya kituo cha kijeshi katika vitongoji vya mji mkuu wa Saudia, Riyadh.
Rais aliyejiuzulu Yemen ni kibaraka wa Saudia na msaliti wa nchi yake
Shambulizi hilo lililofanikiwa lina ujumbe muhimu sana. Kombora hilo la balistiki ambalo lililenga kituo cha kijeshi cha al-Mazahamiah lina uwezo wa kuruka umbali wa kilomita 800 sambamba na kuwa na uwezo mkubwa wa kuharibu eneo linalolengwa. Kombora hilo ambalo limetajwa kuwa Borkan 1 linaliwezesha Jeshi la Yemen kulenga kwa urahisi Riyadh, mji mkuu wa Saudia.
Taarifa ya pamoja iliyotolewa na  Kitengo cha Makombora katika Jeshi la Yemen na  Kamati za Kujihami za Wananchi wa Yemen imesema kombora hilo limevurumishwa Riyadh kama njia ya kujibu na kulipiza kisasi hujuma na jinai zisizo na kikomo za utawala wa Aal Saud dhidi ya watu wa Yemen. Taarifa hiyo imetahadharisha kuwa shambulizi lijalo litakuwa kali zaidi. Kwa maneno mengine ni kuwa, kuanzia sasa Saudi Arabia haitakuwa mvamizi tu bali pia italazimika kujilinda kutokana na mashambulizi ya Wayemen wanaolipiza kisasi.
Hali kadhalika taarifa hiyo ya vikosi vya ulinzi Yemen imesema kujihami ni haki ya kisheria ya Wayemen.
Hujuma ya Saudia dhidi ya Yemen imesababisha vifo vya Wayemen zaidi ya 12,000 wengi wao wakiwa ni raia wa kawaida hasa wanawake na watoto, huku wengine zaidi ya 35,000 wakijeruhiwa vibaya na asilimia 80 ya miundomsingi ya nchi hiyo  kuharibiwa sambamba na mamilioni ya watu kuwa wakimbizi. Ukatili na unyama huo wa Saudia dhidi ya Yemen kwa hakika ni jinai za kivita na jinai dhidi ya binadamu na kwa msingi huo hatua ya Jeshi la Yemen na Kamati za Kujihami za Wananchi ya kuvurumisha kombora la balistiki mjini Riyadh ni mfano wa wazi wa 'haki ya kisheria ya kujihami'. Hii ni haki ambayo imebainishwa wazi katika kipengee cha 51 cha Hati ya Umoja wa Mataifa.
Nyumba ya raia iliyolengwa na dege za kivita za Saudia nchini Yemen
Jambo lenye umuhimu mwingine hapa ni hili kuwa, Mansour Hadi, rais wa Yemen aliyejiuzulu na kutoroka nchi kwa mara nyingine ameonyesha usaliti wake kwa watu na nchi ya Yemen.
Katika hali ambayo ndege za kivita za Saudia zimedondosha mabomu katika maeneo mbali mbali ya Yemen kama njia ya kubainisha hasira baada ya kushambuliwa mji wa Riyadh, Mansour Hadi anayeishi uhamishoni mjini humo amekutana na Mohammad Bin Salman na kuishukuru Saudia kwa kuendelea kuunga mkono serikali yake iliyojiuzulu. Pamoja na uhaini wake huo, Mansour Hadi angali anajitambua kuwa eti ndiye rais halali wa Yemen!

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages