Thursday, February 9, 2017

GAMBIA KUBATILISHA MSIMAMO WA KUJITOWA ICC

Gambia itabatilisha msimamo wake wa kujitoa katika Mahakama ya Jinai ya Kimataifa mjini The Hague. Afisa mmoja wa Umoja wa Ulaya alisema hayo leo, baada ya Rais wa zamani Yahya jammeh kuanza mchakato wa kujitoa mwaka jana. Kamishna wa Umoja wa Ulaya anayehusika na ushirikiano na maendeleo Venev Mimica alitangaza taarifa hiyo kupitia mtandao wa Tweeter , baada ya mazungumzo na Rais mpya Adama Barrow, akiuita uamuzi huo ni " habari njema." Gambia ilikuwa moja wapo ya nchi tatu za kiafrika kutangaza azma ya kujitoa katika Mahakama hiyo ya Kimataifa. Nyengine ni Burundi na Afrika Kusini. Nchi nyingi za Kiafrika zimelalamika kwamba Mahakama hiyo imekuwa na upendeleo na kuwaandama tu Viongozi wakiafrika.

No comments:

Post a Comment