Sunday, February 26, 2017

RAIS YOWERI MUSEVENI AMALIZA ZIARA YAKE YA SIKU MBILI NA KUREJEA NCHINI KWAKE

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpokea Mgeni wake Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Terminal 1 kwa ajili ya kurejea nchini kwake Uganda mara baada ya kumaliza ziara yake ya siku mbili hapa nchini. 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na mgeni wake Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Terminal 1 kabla ya kuondoka  ma kurejea nchini kwake. 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na mgeni wake Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Terminal 1 kabla ya kuondoka  ma kurejea nchini kwake.


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni wakati nyimbo za Mataifa mawili zilipokuwa zikipigwa katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Terminal 1.
 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakifurahia jambo wakati walipokwenda kumsindikiza Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Terminal 1.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na mgeni wake Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni kabla hajapanda ndege na kurejea nchini kwake Uganda mara baada ya kumaliza ziara yake hapa nchini.
 Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan akiagana na Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni kabla hajapanda ndege na kurejea nchini kwake Uganda mara baada ya kumaliza ziara yake hapa nchini.
 Mmoja wa Mtumbuizaji Uwanjani hapo akionesha umahiri wake wa kupuliza Tarumbeta. 
Benderea za Matifa mawili ya Uganda na Tanzania zikipepea Uwanjani hapo. (PICHA NA IKULU)

RAIS MUSEVENI ATEMBELEA VIWANDA VYA BAKRESA JIJINI DAR ES SALAA LEO, AWAKARIBISHA WATANZANIA KUWEKEZA NCHINI UGANDA

 Afisa Mtendaji Mkuu wa Kundi la Makampuni ya Bakhresa  Bw. Salim Aziz akimkabidhi zawadi Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni baada ya kumaliza ziara katika viwanda vya Kuzalisha Unga wa Ngano Cha Bakhresa Food Products kilichopo Buguruni  na  Kiwanda cha Juisi cha Azam kilichopo Vingunguti Jijini Dar es Salaam leo. 
Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni akifurahia zawadi aliyopewa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Kundi la Makampuni ya Bakhresa Bw. Salim Aziz (wapili kulia) mara baada ya kumaliza ziara katika viwanda vya Kuzalisha Unga wa Ngano Cha Bakhresa Food Products kilichopo Buguruni  na  Kiwanda cha Juisi cha Azam kilichopo Vingunguti Jijini Dar es Salaam leo. Kulia kwake ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt. Augustine Mahiga.
 Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni akishukuru kwa kupewa zawadi ya maboksi ya Juisi za Azam mara baada ya kumaliza ziara katika Kiwanda cha Kuzalisha Unga wa Ngano Cha Bakhresa Food Products kilichopo Buguruni  na  Kiwanda cha Juisi cha Azam kilichopo Vingunguti Jijini Dar es Salaam leo. Kulia kwake ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt. Augustine Mahiga na Afisa Mtendaji Mkuu wa Kundi la Makampuni ya Bakhresa Bw. Salim Aziz (kulia).

 Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa Ziara ya Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni katika viwanda vya Kuzalisha Unga wa Ngano Cha Bakhresa Food Products kilichopo Buguruni  na  Kiwanda cha Juisi cha Azam kilichopo Vingunguti Jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Kundi la Makampuni ya Bakhresa Bw. Salim Aziz.

 Rais wa Uganda Mhe.Yoweri Museveni(wapili kushoto) akiulizia jambo wakati wa ziara yake katika viwanda vya Kuzalisha Juisi cha Azam kilichopo Vingunguti jijini Dar es Salaam leo. Kutoka kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Kundi la Makampuni ya Bakhresa Bw. Salim Aziz, Mkurugenzi wa Mahusiano wa Kundi la Makampuni ya Bakhresa Hussein Sufiani na Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Dkt. Adelhelm Meru.
 Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni akishukuru kwa kupewa zawadi ya maboksi ya Juisi za Azam mara baada ya kumaliza ziara katika Kiwanda cha Kuzalisha Unga wa Ngano Cha Bakhresa Food Products kilichopo Buguruni  na  Kiwanda cha Juisi cha Azam kilichopo Vingunguti Jijini Dar es Salaam leo. Kulia kwake ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt. Augustine Mahiga na Afisa Mtendaji Mkuu wa Kundi la Makampuni ya Bakhresa Bw. Salim Aziz (kulia).
 Mkurugenzi wa Mahusiano wa Kundi la Makampuni ya Bakhresa akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa Ziara ya Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni katika viwanda vya Kuzalisha Unga wa Ngano Cha Bakhresa Food Products kilichopo Buguruni  na  Kiwanda cha Juisi cha Azam kilichopo Vingunguti Jijini Dar es Salaam leo.
Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni(mweneye kofia) akiwa katika picha ya pamoja na menejimenti ya Kundi la Makampuni ya Bakhresa mara baada ya kumaliza ziara katika Kiwanda cha Kuzalisha Unga wa Ngano Cha Bakhresa Food Products kilichopo Buguruni  na  Kiwanda cha Juisi cha Azam kilichopo Vingunguti Jijini Dar es Salaam leo.
Picha zote na: Frank Shija – MAELEZO.
 Afisa Mtendaji Mkuu wa Kundi la Makampuni ya Bakhresa  Bw. Salim Aziz akimtambulisha Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni kwa wafanyakazi wa alipofanya ziara katika viwanda vya Kuzalisha Unga wa Ngano Cha Bakhresa Food Products kilichopo Buguruni  na  Kiwanda cha Juisi cha Azam kilichopo Vingunguti Jijini Dar es Salaam leo.  
 Mkurugenzi wa Mahusiano wa Kundi la Makampuni ya Bakhresa akimwelezea jambo Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni kwa wafanyakazi wa alipofanya ziara katika Kiwanda cha Kuzalisha Unga wa Ngano Cha Bakhresa Food Products kilichopo Buguruni  na  Kiwanda cha Juisi cha Azam kilichopo Vingunguti Jijini Dar es Salaam leo. 
 Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni akiwasili katika Kiwanda cha Juisi cha Azam kilichopo Vingunguti Jijini Dar es Salaam leo.Kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Kundi la Kampuni za Bakhresa  Bw. Salim Aziz.
 Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Museveni akiangalia namna Juisi ya Azam inavyotengenezwa alipofanya ziara katika Kiwanda hicho leo Jijini Dar es Saalam. Kulia ni Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe.Charles Mwijage. Baadhi ya wafanyakazi wa Kundi la Makampuni  ya Bakhresa wakifurahia ugeni wa Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Museveni(hayupo pichani) wakati wa ziara yake katika viwanda vya Kuzalisha Juisi cha Azam kilichopo Vingunguti jijini Dar es Salaam leo.

MAZOEZI YA KIJESHI YA IRAN YANA UJUMBE WA AMANI

Kamanda wa Jeshi la Majini la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema lengo la mazoezi ya majini ya Wilayat 95 ni kutuma ujumbe wa amani na urafiki kwa nchi za eneo sambamba na kuinua kiwango cha kujihami Iran.
Admeri Habibullah Sayyari Kamanda wa Jeshi la Majini la Iran aliyasema hayo Jumamosi usiku katika mahojiano na Kanali ya Pili ya Televisheni ya Iran. Amesema awamu ya mwisho ya mazoezi ya kijeshi yaliyopewa jina la "Wilayat 95" yanaanza leo Jumapili na kuongeza kuwa, upana wa eneo la mazoezi ni karibu kilomita mraba milioni mbili kuanzia Lango Bahari la Hormoz kuelekea  Bahari ya Oman hadi Kaskazini mwa Bahari ya Hindi yapata daraja 10 kutoka mstari wa ikweta.
Admeri Sayyari amesema, kati ya malengo ya mazoezi hayo ni kuwapa wanajeshi vijana uzoefu wa kikazi na kufanyia majaribio silaha mbali mbali. Aidha ametaja lengo jingine la luteka hiyo kuwa ni kudumisha amani katika eneo na kukabiliana na ugaidi pamoja na uharamia na kuongeza kuwa: "Hadi sasa misafara ya meli za kivita za Iran imezisaidia meli za nchi 25 duniani zikiwemo za Ufaransa, Uingereza na Marekani katika kukabiliana na maharamia.
Manowari ya Iran katika mazoezi ya kivita
Admeri Sayyari amesema tokea mwaka 2008 hadi sasa, manowari za Iran zimesindikiza meli za mafuta na za kibiashara zipatazo 3,850  katika eneo la Bahari ya Hindi na Babul Mandab.
Admeri Sayyari amesema Iran ina uhusiano mzuri na nchi zote zenye mipaka katika Bahari ya Hindi na Bahari ya Kaspi na kuongeza kuwa, mwaka 2018 Iran itakuwa mwenyeji wa makamanda wa majeshi ya majini ya nchi zinazopakana na Bahari ya Hindi.

UN YATAKA UCHAGUZI UFANYIKE KUHUSU MAUAJI KASAI, DRC

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limetoa taarifa likilaani vikali matukio ya utumiaji mabavu yaliyotokea katika miezi ya hivi karibuni huko Kasai, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, na kuihimiza serikali ya nchi hiyo kuchunguza mara moja matukio hayo.
Katika taarifa, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa  limeashiria ghasia katika miezi ya hivi karibuni huko  Kasai na kutokana na hali hiyo, wajumbe wa Baraza hilo wamesema wana hofu kutokana na ukiukwaji mkubwa wa sheria za kibinadamu za kimataifa kukiwemo wanamgambo kutumikisha watoto vitani na jeshi la serikali kuua raia.
Wamesema vitendo vyote hivyo vinaweza kuwa uhalifu wa kivita chini ya sheria za kimataifa hivyo wametaka serikali iwajibike kulinda raia na ijizuie kutumia nguvu za kijeshi kupita kiasi.
Wameitaka serikali kufanya uchunguzi usioegemea upande wowote na wahusika wafikishwe mbele ya sheria huku wakisema kuwa ujumbe wa umoja huo DRC, MONUSCO utakuwa tayari kusaidia iwapo utaombwa kufanya hivyo.
Kuhusu uchaguzi, wajumbe hao wamesisitiza umuhimu wa serikali ya DRC na wadau wa kitaifa kuchukua hatua zote muhimu za kuandaa uchaguzi huo bila kuchelewa na kuhakikisha mazingira ni salama kwa uchaguzi huru na wa haki.
Waasi nchini DRC
Wametoa wito kwa wadau wa maendeleo wa DRC kusaidia ili kufanikisha uchaguzi huku wakisema wako tayari kufanikisha utekelezaji wa makubaliano ya tarehe 31 mwezi Disemba mwaka jana yanayohusisha pia uchaguzi.
Siku chache zilizopita, Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa Zeid Ra’ad Al Hussein aliitaka serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kuchukua hatua za haraka kusitisha ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu, ikiwa ni pamoja na mauaji ya raia yanayofanywa na jeshi la nchi hiyo. Alisema kuna habari za kuaminika na madai ya ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu katika eneo la Kasai  ya Kati na Mashariki na jimbo la lomami, huku kukiwa na kuzorota kwa kasi hali ya usalama na watu wakilengwa na askari kwa madai ya kuwa na uhusiano na wanamgambo wa ndani.

WATOTO 6 WAUAWA SHAHIDI KATIKA HUJUMA YA SAUDIA YEMEN

Watu wasipoungua 8 wakiwemo watoto sita wameuawa shahidi katika hujuma ya hivi karibuni ya ndege za kivita za Saudia katika maeneo mbali mbali nchini Yemen.
Kwa mujibu wa taarifa, siku ya Jumamosi ndege za kivita za Saudia zilishambulia mji wa bandarini wa Mukha katika Bandari ya Sham yapata kilomita 346 kusini mwa mji mkuu, Sana'a ambapo watoto watano wameuawa shahidi.
Aidha mke na mume na mtoto wao wamepoteza maisha baada ya ndege za kivita za Saudia kudondosha mabomu katika nyumba moja iliyo katika kijiji cha Manjada katika mkoa wa Dhamar, kusini magharibi mwa Yemen.
Hali kadhalka jana jioni ndege za kivita za Saudia zililenga kituo cha kijeshi cha Khalid katika Wilaya ya Mawza kaskazini magharibi mwa mkoa wa Ta'izz.
Katika kulipiza kisasi jinai hizo za Saudia, wapiganaji wa Kamati za Wananchi wamewapiga risasi na kuwaua wanajeshi wawili wa Saudi Arabia katika eneo la mkoa Jizan. 
Makao ya raia yaliyoharibiwa kwa mabaomu ya ndege za kivita za Saudi
Wakati huo huo Mkurugenzi wa Utalii Yemen Abdulrahman al-Na'mi amesema jeshi la Saudia limehujumu na kuharibu zaidi ya maeneo 200 ya kitalii nchini Yemen na kuisababishia nchi hiyo hasara ya dola bilioni 4.5 tokea Machi mwaka 2015 hadi sasa. Aidha amesema hujuma hiyo ya Saudia Yemen imepeleke karibu watu 90,000 kupoteza ajira katika sekta ya utalii.
Saudia, kwa kushirikiana na waitifaki wake, ilianzisha hujuma za kila upande dhidi ya Yemen tarehe 26 Machi mwaka 2015 kwa lengo la kumrejesha madarakani kibaraka wake Abdrabbuh Mansur Hadi rais wa zamani wa Yemen ambaye alijiuzulu nafasi hiyo na kukimbilia Saudia.
Hata hivyo licha ya Riyadh kufanya mauaji na uharibifu mkubwa nchini Yemen, imeshindwa kufikia malengo yake haramu nchini humo.

Saturday, February 25, 2017

UHUSIANO KATI YA TRUMP NA WANAHABARI WAZIDI KUZOROTA

Rais wa Marekani Donald Trump amesema hatahudhuria dhifa ya chakula cha jioni inayoandaliwa na chama cha waandishi wa habari wanaoripoti matukio ya Ikulu.
Washington Donald Trump beim traditionellen Korrespondenten-Galadinner im Weißen Haus (Getty Images/L. Busacca)
Tangazo la Trump linakuja siku moja baada ya kuwashutumu vikali wanahabari kwa kuwataja kuwa ni adui wa watu kwa kudai wanaeneza taarifa za uongo na za kupotosha. Kiongozi huyo mpya wa Marekani pia amewataja wanahabari kuwa chama cha upinzani nchini Marekani. Dhifa hiyo iliyoanzishwa mwaka 1921, huwa inahudhuriwa na watu mashuhuri, wanasiasa wa Marekani na wanahabari.
Rais wa chama cha waandishi wa habari wa Ikulu ya White House WHCA Jeff Mason amesema dhifa hiyo itaendelea kama ilivyopangwa kwani ni desturi ya kusherehekea mchango muhimu unaotekelezwa na mashirika ya habari katika taifa lililo huru, kusherehekea uhuru, kuangazia mafanikio ya uandishi habari katika ulingo wa kisiasa na kuwatambua wanafunzi bora wanaosomea uandishi ambao wanawakilisha kizazi kijacho cha tasnia hiyo ya habari.
Washington Barack Obama beim traditionellen Korrespondenten-Galadinner im Weißen Haus (Getty Images/O. Douliery-Pool) Rais wa zamani wa Marekani Barack Obama katika dhifa ya 2016
Trump awataja wanahabari wapinzani
Msemaji wa Ikulu Sean Spicer mnamo siku ya Ijumaa aliwazuia wanahabari wa mashirika kadhaa kuhudhuria kikao cha wanahabari katika Ikulu. Wanahabari wa Mashirikia ya CNN, New York Times, Politico, Los Angeles Times na Buzzfeed hawakuruhusiwa kuhudhuria kikao cha wanahabari katika ofisi ya msemaji wa Ikulu ya Rais wa Marekani.
Katika kipindi cha kampeini mwaka jana, kundi la Trump liliyapiga marufuku mashirika kadhaa likiwemo gazeti la Washington Post na Buzzfeed dhidi ya kuripoti katika mikutano ya kampeini likiyashutumu kwa upotoshaji ba kueneza habari za uongo.
Spicer amesema Ikulu ya Marekani inapanga kupambana dhidi ya kile alichokitaja kuangaziwa kionevu na vyombo vya habari. Msemaji huyo wa Ikulu ameeleza kuwa hawatakaa tu na kuruhusu taaarifa za uongo na za kupotosha zikitolewa.
Uhuru au upotoshaji wa habari?
Hatua hiyo ya utawala wa Trump kuyashambulia mashirika ya habari nchini Marekani imeashutumiwa vikali na makundi ya wanahabari na vyomvo hivyo vya habari.
Taarifa kutoka kwa mhariri mkuu wa The New York Times Dean Baquet ilisema jambo kama hilo halijawahi kutokea katika Ikulu ya Rais ya White House katika historia yao ndefu ya kuripoti taarifa kutoka tawala chungu nzima kutoka vyama tofauti vya kisiasa nchini Marekani.
USA Weißes Haus - Sean Spicer (picture-alliance/newscom/UPI Photo/P. Benic) Msemaji wa Ikulu ya Rais Sean Spicer
Baquet alisema wanapinga vikali kuzuiwa kwa gazeti lao na mashirika mengine ya habari na kuongeza kuruhusiwa kwa vyombo hivyo kuwa na uhuru na kuangazia matukio ya serikali iliyo wazi bila shaka ni muhimu kwa maslahi ya taifa.
Wakati wa kampeini zake kuingia madarakani, Trump mwenye umri wa miaka 70 aliyashutumu vikali mashirika makuu ya habari ya Marekani kwa kuwa na upendeleo na amezidisha shutuma hizo baada ya kuingia madarkani kwa kudai wanahabari wanaangazia zaidi mapungufu yake badala ya kuangazia mafanikio yake.
Stephen Bannon, mkuu wa mipango na mshauri mwandamizi wa Trump ambaye pia ni mkuu wa tovuti ya kihafidhina ya Breitbart, amebadhiri kuwa uhusiano kati ya utawala huo mpya wa Marekani na wanahabari ambao amewataja wapinzani utazidi tu kuwa mbaya jinsi rais huyo wa Marekani anavyozidi kutoa ajenda zake.

WASHIRIKA WA MUGABE KUSHIRIKI SHEREHE YA KUZAKIWA

Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe aliyefikisha miaka 93 wiki hii, leo anaadhimisha siku yake ya kuzaliwa kwa kufanya sherehe ya kifahari itakayohudhuriwa na maelfu ya wanaomuunga mkono nje ya mji wa pili kwa ukubwa nchini humo wa Bulawayo. Chama tawala, ZANU-PF kinaandaa sherehe ya kiongozi huyo aliyeko madarakani tangu mwaka 1980 na utawala wake ukiwa umegubikwa na ukandamizaji wa wapinzani, udanganyifu wa kura na kuanguka kwa uchumi. Kiongozi huyo wa taifa mwenye umri mkubwa zaidi duniani kwa sasa, amekuwa akisherehekea siku hii kwa wiki nzima, huku kituo cha televisheni cha taifa kikimmwagia sifa kemkem na pongezi. Sherehe hiyo inagharimu Dola Milioni 1, hatua iliyowaghadhabisha Wazimbawe wengi kufuatia upungufu wa chakula unaoikabili nchi hiyo. Kufanyika kwa sherehe hiyo katika shule ya Matobo kumewachukiza wakazi wa eneo hilo kwa kile kinachoaminika kuwa wahanga wa machafuko dhidi ya wapinzani chini ya utawala wake katika miaka ya 1980 walizikwa eneo hilo.

PENCE ASEMA WAHAFIDHINA WANA FURSA YA KIHISTORIA

Makamu wa Rais wa Marekani Mike Pence amesema Marekani imepata fursa ya kipekee kutatua matatizo yanayoikabili nchi hiyo kwa kutumia majibu ya chama cha Republican baada ya chama hicho kudhibiti urais na bunge.
US Wahl Mike Pence Vizepräsident in Manchester (Reuters/J. Ernst)
Pence aliyasema hayo katika mkutano wa vuguvugu la wahafidhina unaofanyika mjini Oxon Hill ambao unatarajiwa kuhutubiwa na rais Donald Trump hii leo. Pence aliutaja ushindi wa Trump katika uchaguzi wa mwaka jana kuwa ni fursa ya maisha na hivyo kuwataka wanaharakati wa kihafidhina kutoiharibu fursa hiyo.
Makamu wa rais Pence alisema utawala mpya wa Trump umewapa fursa wahafidhina kuonyesha kwamba majibu yao ndiyo sahihi kwa Marekani. Pence alisema utawala huo mpya utaiondoa sheria ya huduma za afya na kuanzisha nyingine mbadala, akisema jinamizi la taifa la Obamacare linakaribia kufika mwisho. Lakini aliongeza kuwa wahafidhina wanapaswa kujiandaa na mapambano dhidi ya Wademocrat.
USA National Harbor, Maryland Steve Bannon bei CPAC (Getty Images/A. Wong) Mkuu wa shughuli za ikulu ya White House Reince Priebus akizungumza wakati wa mkutano wa CPAC, Maryland.
"Ndani ya timu hii, sisi wahafidhina tunayo fursa ambayo inakuja kila baada ya vizazi vichache, au inaweza kuja mara moja tu katika maisha. Marafiki zangu, hii ndiyo  fursa tuliyoisubiri kwa muda mrefu. Huu ndiyo wakati wa kuonyesha kwa mara nyingine kwamba majibu yetu ndiyo majibu sahihi kwa Marekani. Jeshi imara, nafasi zaidi za ajira, kodi kidogo, kuheshimu katiba na maadili yalioifanya Marekani kuwa taifa kubwa na imani kubwa katika uzuri wa watu wa Marekani," alisema Pence.
Mashaka ya wahafidhina kwa Trump
Mapema mkuu wa shughuli za ikulu Reince Priebus aliomba uvumilivu na umoja, akiwasihi wanaharakati kutofuja udhibiti wa Warepublican wa mabaraza yote ya bunge pamoja na ikulu ya White House. Mshauri wa Trump Steve Bannon aliwasilisha hoja ya kuwa mkakati wa utawala wenye msingi wake katika kupunguza utitiri wa sheria na uzalendo wa kiuchumi katika kujadili mikataba mipya ya kibiashara.
Utetezi wa Priebus umetambua mashaka ya wahafidhina kuhusu rais huyo mpya, mwanachama wa zamani wa chama cha Democratic ambaye huko nyuma alikuwa akizomewa aktika mkutano huo. Trump ameonyesha mara kwa mara kuwa hatoi kipaumbele kwa masuala ya kijamii ambayo wahafidhina wengi wanayapa umuhimu, na pendekezo lake la uwekezaji mkubwa katika miundombinu limetia mashaka dhamira yake ya kupunguza matumizi ya serikali.
USA CPAC-Treffen - Konferenz der Konservativen (DW/M. Shwayder) Wajumbe wakielekea kwenye mkutano wa CPAC
Lakini wakati ambapo Mrepublican akikalia kiti cha rais kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka nane, wanaharakti wengi wanasema wanahisi wana nguvu na wako tayari kumpa nafasi. Vuguvugu la wanaharakati wa kihafidhina lililoanzishwa muongo mmoja uliopita limekuwa kama kamati ya ushawishi.
Rais Trump anatarajiwa kuhutubia mkutano huo ulioingia katika siku ya tatu leo, akilenga kuimarisha ushawishi wake katika jukwaa ambalo kw amuda mrefu limetafuta njia za kubadilisha mfumo wa sheria za kodi za Marekani, kupunguza utitiri wa sheria za udhibiti wa biashara na kufuta sheria ya huduma za afya ya rais wa zamani wa Demcratic Barack Obama.

MERKEL AUPONDA MPANGO WA SPD

Kansela Angela Merkel wa Ujerumanin Jumamosi Feb 25, 2017 awashutumu washirika wake katika serikali ya mseto kwa kupendekeza marekebisho kwa magaeuzi ya ustawi wa jamii.
Stralsund Angela Merkel auf CDU-Landesvertreterversammlung (picture-alliance/dpa/S. Sauer)
Kansela Angela Merkel wa Ujerumanin Jumamosi Feb 25, 2017 awashutumu washirika wake katika serikali ya mseto kwa kupendekeza marekebisho kwa magaeuzi ya ustawi wa jamii ambayo yanapongezwa kwa kuchochea mafanikio ya uchumi wa taifa.
Kwa mujibu wa uchunguzi wa maoni mgombea wa chama cha SPD amempiku Merkel wakati nchi ikielekea katika uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika mwezi wa Septemba mwaka huu. Chama hicho kwa miaka kadhaa kilikuwa nyuma ya muungano wa wahafidhina wa Merkel katika uchunguzi wa maoni. Lakini kuungwa mkono kwa chama hicho cha sera za wastani mrengo wa kushoto kumeongezeka tokea kilipomteuwa spika wa zamani wa bunge la Ulaya kuwa mgombea wao mwishoni mwa mwezi wa Januari.
Martin Schulz alitaka kuuvutia upande wa sera za mrengo wa kushoto wa chama chake hapo Jumatatu kwa kusema marekebisho yanahitajika kwa mageuzi ya  "Agenda 2020"
ambayo yaliandaliwa na Kansela Gerhard Schroeder wa chama cha SPD lakini ikamghariu wadhifa wake huo na kukigawa chama.
Mageuzi hayo yaliyozinduliwa mwaka 2013 yalisababisha wanachama wengi wa SPD kujitowa na kujiunga na chama cha sera kali za mrengo wa kushoto Die Linke.
Mpango wa mageuzi wasifiwa
Stralsund Angela Merkel auf CDU-Landesvertreterversammlung (picture-alliance/dpa/S. Sauer) Kansela Angela Merkel akiwa katika jimbo lake la uchaguzi la Stralsund na kiongozi wa wabunge wa CDU Vincent Kokert katika bunge la jimbo la Mecklenburg-Western Pomerania.
Lakini Merkel ameusifu mpango huo wa mageuzi katika kampeni ya uchaguzi kwenye jimbo lake la uchaguzi la Sraklsund kaskazini mwa Ujerumani Jumamosi kwa kusema "Ndio maana nilisema wakati nilipoingia madaraka miaka 11 iliopita kwamba Kansela Schroeder ametowa mchango mkubwa kwa Ujerumani kwa agenda yake hiyo ya 2010.
Amesema wahafidhina wamefanya baadhi ya marekebisho ya mageuzi tokea mwaka 2005 wakati walipounda serikali ya mseto lakini ilishikilia kiini cha mpango huo kwa sababu uliwapatia ajira watu wengi na kiwango cha watu wasiokuwa na kazi kikapunguwa kwa nusu tokea mwaka 2005.
Merkel amesema lakini siku hizi chama cha SPD hakitaki kuutangaza mpango huo kuwa ni wa mafanikio.Amesema Ujerumani inahitaji kuwa na mdahalo kuhusu Agenda 2025 na amekituhumu chama cha SPD kwa kuendelea kuangalia kipindi chake kilichopita na sio mustakbali wake.
Pia amesema ni muhimu kuiandaa Ujerumani kwa mabadiliko makubwa kupitia utandawazi na kutowa wito kwa makampuni yanayotumia fedha kwa ajili ya utafiti yapunguziwe kodi ili kuzishajiisha kampuni ndogo ndogo zifanye utafiti zaidi.
Malipo ya uzeeni yatetewa
SPD-Kanzlerkandidat Martin Schulz (picture alliance/dpa/C. Charisius) Martin Schultz kiongozi wa chama cha SPD na mgombea ukansela kwa tiketi ya chama hicho.
Katika hotuba yake hapo Jumatatu Schulz alizungumzia juu ya kuwahami wafanyakazi wazee pamoja na kuanzisha vikwazo kwa mikataba ya kazi ya muda na kutetea malipo ya uzeeni.
Waajiri wanasema jambo hilo litaumiza uchumi.
Schulz ameiambia kampuni ya vyombo vya habari Redaktionsnetzwerk Deutchland  (RND) kwamba anataraji  uchaguzi wa Septemba 24 utakuwa wa mchuano mkali.
Schulz amesema zaidi ya asilimia 20 ya wapiga kura huaumuwa siku kumi za mwisho wakati asilimia mbili hadi tatu huamuwa siku ya uchaguzi yenyewe na kwamba matokeo huenda yakategemea asili hiyo mbili au tatu ya siku ya mwisho

Friday, February 24, 2017

ZUMA: AFRIKA KUSINI ITARUHUSU UTAIFISHAJI WA ARDHI BILA YA FIDIA

Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini amesema leo kuwa nchi hiyo itazifanyia marekebisho sheria zake ili kuruhusu utaifishaji wa ardhi bila ya kuwalipa fidia wamiliki wa ardhi hizo, katika kipindi hiki ambapo nchi hiyo inajaribu kuharakisha zoezi la kuwagawia tena ardhi raia weusi walio wengi wa nchi hiyo.
Itafahamika kuwa sehemu kubwa ya ardhi ya Afrika Kusini inamilikiwa na wazungu kwa zaidi ya miongo miwili baada ya kumalizika utawala wa ubaguzi wa rangi nchini humo (Apartheid). Rais Zuma amesema katika hotuba yake akiashiria sera za kilimo za serikali yake kuwa, wanahitaji kuchukua hatua madhubuti zitakazobadili uchumi wa nchi hiyo kwa haraka, likiwemo suala la umiliki wa ardhi.
Moja ya mashamba ya zabibu yanayomilikiwa na wazungu nchini Afrika Kusini 
Wachambuzi wa mambo wanasema kuwa msimamo huo mkali ulioonyeshwa na chama tawala ANC unajiri sambamba na miito iliyotolewa na chama cha upinzani cha Economic Freedom Fighters ambacho kimetaka kutaifishwa ardhi zinazomilikiwa na wazungu huko Afrika Kusini. Wachambuzi hao pia wanasema kuwa serikali ya Afrika Kusini imechukua hatua hiyo ili kuungwa mkono kisiasa chama tawala katika ngome za vijijini kabla ya kufanyika uchaguzi wa ndani ya chama mwezi Disemba mwaka huu.

MAPIGANO YA KIKABILA YA UMWAGAJI DAMU MASHARIKI MWA KONGO

Makumi ya watu wameuawa hadi sasa tangu kuanza tena mapigano katika mkoa wa Tanganyika nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo mwezi Julai mwaka jana.
Richard Ngoie Kiatngala, Gavana wa mkoa wa Tanganyika mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo  amesisitiza wakati wa kuanza kikao cha kujadili amani na suluhu kati ya makabila ya Luba (Bantu) na Pygmees kuwa, katika mapigano hayo watu 150 wameuawa hadi sasa, 200 wamejeruhiwa, shule 400 zimebomolewa na vijiji 422 kuchomwa moto. Gavana huyo wa mkoa wa Tanganyika ameongeza kuwa kesi 200 za ubakaji zimethibitishwa kutokea kufuatia mapigano hayo ya kikabila; huku asilimia 76.4 ya wakazi wa mkoa wa Tanganyika wakikabiliwa na uhaba wa chakula na mlipuko wa maradhi ya kipindupindu na surua. 
Watu wa kabila la Pygmees wanaodaiwa kuvichoma moto vijiji vya jamii ya Luba  
Gavana wa mkoa wa Tanganyika ametaka kurejeshwa haraka amani na utulivu katika mkoa huo. Wakati huo huo Emmanuel Ramazani Shadary Waziri wa Mambo ya Ndani na Usalama wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo amesema kuwa hali ya mkoa wa Tanganyika inatia wasiwasi na kuzitolea mwito pande zinazozozana kufanya mazungumzo. Mkoa wa Tanganyika umekumbwa na mapigano ya umwagaji damu baina ya makabila mawili ya Luba na Pygmees tangu miezi kadhaa iliyopita hadi sasa.

MAREKANI YAJATIBU KUTULIZA WASIWASI MEXICO

Maafisa wa Marekani wameihakikishia Mexico kuwa hakutakuwa na ufukuzwaji wa kimakundi au kulitumia jeshi la Marekani kuwatimuwa wahamiaji haramu, walioelezwa na Rais Donald Trump kuwa watu waovu.
Mexiko US-Außenminister Tillerson auf Besuch mit Amtskollegen Videgaray (Reuters/C. Jasso) Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Rex Tillerson akisalimia na mwenzi wake wa Mexico Luis Videgaray.
Mawaziri wa Marekani - wa mambo ya ndani John Kelly na wa nje Rex Tillerson walikutana na mawaziri wa Mexico walioeleza wasiwasi na kukerwa na msimamo wa kibabe wa Trump kuhusu uhusiano wa kibiashara na uhamiaji na Mexico.
Waziri wa mambo ya nje wa Mexico Luis Videgaray alisema baada ya kukutana na mawaziri Kelly na Tillerson kwamba serikali za mataifa hayo zimechukua hatua muhimu kuelekea njia sahihi. Uhusiano kati ya Marekani na Mexico umekuwa wa mvutano tangu kuapishwa mwezi Januari kwa Donald Trump, ambaye ameapa kukomesha uhamiaji haramu kutoka Mexico.
Sheria kuzingatiwa kufukuza wahamiaji haramu
Wizara ya usalama wa ndani ilitoa maagizo mapya siku ya Jumanne, kuimarisha ukamataji na urejeshwaji wa wahamiaji haramu, wengi wao wakiwa raia wa Mexico. Lakini waziri Kelly aliahidi katika mkutano wa habari mjini Mexico City siku ya Alhamisi, kwamba hakutakuwa na urejeshwaji wa makundi ya watu.
Mexiko US-Außenminister Tillerson auf Besuch mit Amtskollegen Videgaray und US-Heimatschutzminister John Kelly (Getty Images/AFP/R. Schemidt) (Kushoto - Kulia) Waziri wa usalama wa ndani wa Marekani John Kelly, waziri wa mambo ya nje wa Mexico Luis Videgaray na waziri wa mambo ya nje wa Marekani Rex Tillerson baada ya kuhutubia mkutano wa pamoja na waandishi habari.
"Hakutakuwepo, na narudia, hakuna kufukuza watu kimakundi. Kila kitu tunachokifanya katika wizara ya usalama wa ndani kitafanywa kisheria, na kuzingatia haki za binadamu katika mfumo wa sheria wa Marekani. Urejeshaji wote utafuata mfumo wetu wa sheria," alisema Kelly katika mkutano na waandishi habari mjini Mexico City.
Akizungumza mapema katika ikulu ya White House, Trump aliuelezea urejeshaji wa makundi ya wahamiaji kuwa operesheni ya kijeshi. Lakini Msemaji wake Sean Spicer baadae akauambia mkutano wa waandishi habari kwamba Trump alikuwa akitumia neno "jeshi" kama kivumishi kumaanisha ufanisi. Au kama Tump mwenye alivyoeleza: Tunawafukuza watu waovu nchini mwetu, na kwa kiwango ambacho hakijawahi kushuhudiwa.
Ujenzi wa ukuta mpakani
Janauri 25, Trump alisaini Amri ya Rais ya kuanza mara moja ujenzi wa ukuta kwenye mpaka wa kusini, wakati ambapo waziri Luis Videgaray alikuwa akiongoza ujumbe wa Mexico kuelekea mjini Washington. Madai ya Trump kwamba Mexico italipia ujenzi wa ukuta huo yalisababisha kufutwa kwa ziara ya rais wa Mexico Enrique Pena Nieto katika ikulu ya White House.
Trump pia ameahidi kuujadili upya mkataba wa biashara huru wa mataifa ya Amerika Kaskazini NAFTA, pamoja na Canada na Mexico, akiulaumu mkataba huo huo wa miaka 23 kwa kuchangia kwa sehemu kutoweka kwa ajira katika sekta ya viwanda ya Marekani.
Washington US-Präsident Trump im Interview (Reuters/J. Ernst) Rais wa Marekani Donald Trump amesababisha mtikisiko mkubwa nchini Mexico tangu alipoingia madrakani Januari 20, 2017.
Tillerson na Kelly baadae walikutana na Rais Pena Nieto, baada ya kukutana na waziri wa mambo ya nje Videgeray pamoja na mawaziri wa mambo ya ndani Miguel Osorio Chong, na waziri wa fedha wa Mexico Jose Antonio Meade. Tillerson alisema baada ya mazungumzo ya mawaziri kwamba Marekani na Mexico zinaunganishwa na dhamira ya pamoja ya kuheshimiwa kwa sheria na taratibu kwenye mpaka wao wa pamoja.
Wakati huo huo, watu kadhaa wengi wao wakiwa Wamarekani waliandamana mbele ya ubalozi wa Marekani wakitaka kusitishwa kwa vita vya maneno vya Trump dhidi ya Mexico. Katika hatua ambayo yumkini imelenga kuitia kishindo zaidi Mexico, Trump ameyagisha mashirika ya serikali ya Marekani kuhesabu ni misaada kiasi gani wanatoa kwa nchi hiyo.
Pia ameahidi kuziadhibu kampuni za Marekani zinazozalisha bidhaa zake nchini Mexico, na ametishia kuzuwia marejesho ya fedha za Wamexico wanaofanya kazi Marekani.

Thursday, February 23, 2017

MAZUNGUMZO YA AMANI YA SYRIA YAFUNGULIWA GENEVA

Mazungumzo ya amani ya Syria chini ya usimamizi wa Umoja wa Mataifa yanaendelea jijini Geneva, miezi kumi baada ya kusambaratika kuhusiana na umwagaji damu unaoendelea katika nchi hiyo iliyoharibiwa na vita
Kasachstan Syrien Friedensgespräche in Astana (picture-alliance/abaca/A. Raimbekova)
Mjumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Syria Staffan de Mistura alifanya mikutano tofauti na wawakilishi wa ujumbe wa serikali na upinzani leo asubuhi katika ofisi za Umoja wa Mataifa nchini Uswisi. Siku moja kabla, Mwanadiplomasia huyo alipuuza matumaini ya kupatikana makubaliano ya moja kwa moja katika mazungumzo hayo, lakini pande zote zinafahamu kuwa mienendo nchini Syria imebadilika tangu mazungumzo yaliandaliwa mara ya mwisho Geneva mwezi Aprili.
De Mistura anataka pande zote kujadili uwezekano wa kuundwa serikali ya pamoja ya mpito, katiba mpya na kuandaliwa uchaguzi. Duru za upinzani zimesema mikutano ya kwanza leo ilihusu ufafanuzi wa ajenda halisi ya mazungumzo hayo. Mmoja wa wajumbe wa upinzani Abdulahad Astepho amesema waasi watakuwa na jukumu kubwa katika duru hii ya mazungumzo.
Schweiz Genf Staffan de Mistura (Getty Images/AFP/F. Coffrini) De Mistura asema kuna matumaini madogo kwenye mazungumzo hayo ya amani ya Syria, jijini Geneva
Mazungumzo ya Geneva yanakuja baada ya mashauriano ya Astana, mji mkuu wa Kazakhstan, ambayo yaliratibiwa kwa kiasi kikubwa na Uturuki, mshirika wa karibu wa upinzani katika vita hivyo vya wenyewe kwa wenyewe, na Urusi, ambayo mashambulizi yake ya angani yanawasaidia wanajeshi wa sewrikali ya Rais Bashar al-Assad. Ni duru ya nne ya mazungumzo yanayosimamiwa na Umoja wa Mataifa tangu mapema mwaka jana.
Wakati hayo yakijiri, wanaharakati wameripoti leo kutokea mashambulizi makali katika mji wa kusini wa Daraa baina ya wanajeshi wanaoiunga mkono serikali na makundi ya upinzani yanayoongozwa na kundi la al-Qaeda. Mashirika ya habari ya upinzani pia yameripoti mashambulizi ya anga yaliyofanywa na serikali karibu na eneo la Hama, katikati ya Syria.
Serikali inasisitiza kuwa mpango wa kusitisha mapigano hauyalindi makundi yenye mafungamano na mtandao wa  al-Qaeda, wakati waasi wanasema makubaliano waliyosaini mjini Ankara yanayahusisha makundi hayo.
Nalo shirika la Umoja wa Mataifa la Kuwashughulikia Watoto – UNICEF limetoa wito kwa pande zote katika mgogoro wa Syria kuwalinda watoto katika nchi hiyo iliyoharibiwa na vita. Karibu watoto milioni 10 wa Kisyria wanaoteseka moja kwa moja na madhara ya kila siku ya mgogoro huu mkubwa wanataka kitu kimoja tu: amani irejee na wafurahie tena maisha yao ya utotoni.

MKUU WA SHIRIKA LA MAFUTA ATAULIWA KUWA WAZIRI MKUU MPYA WA SOMALIA

Rais mpya wa Somalia, Mohamed Abdullahi Mohamed Farmaajo aliyeapishwa jana mjini Mogadishu amemteua mkurugenzi wa shirika moja la mafuta kuwa Waziri Mkuu mpya wa nchi hiyo.
Shirika la habari la Reuters limetagaza habari hiyo na kuongeza kuwa, Hassan Ali Khaire, Mkurugenzi wa Shirika la Mafuta na Gesi la Soma la Uingereza na ambaye pia ana uraia wa Norway, ndiye Waziri Mkuu mpya wa nchi hiyo ya Pembe ya Afrika.
Tovuti ya radio ya serikali ya Muqdisho.net imewataka wananchi wa Somalia kushirikiana na kufanya kazi bega kwa bega na Waziri Mkuu mpya katika mchakato wa kuundwa serikali mpya.
Hata hivyo baadhi ya wadadisi wa mambo wamesema hatua ya Rais Farmaajo ya kumteua mkuu huyo wa shirika la mafuta, huenda ikaibua suala la mgongano wa maslahi.
Rais Farmaajo akizungumza baada ya kuapishwa
Mohamed Mubarak, mwanaharakati mashuhuri wa kupambana na ufisadi nchini Somalia amepongeza uteuzi wa Ali Khaire na kusisitiza kuwa, kuja kwa Waziri Mkuu huyu mpya kunamaanisha kuwa nchi hiyo haitashuhudia masuala ya rushwa kwa angalau miaka minne ijayo.
Baada ya kuapishwa katika sherehe iliyohudhuriwa na viongozi wa nchi kadhaa za kanda hiyo chini ya hatua kali za ulinzi, rais mpya wa Somalia ameahidi kurejesha heshima ya nchi hiyo ya Pembe ya Afrika lakini pia akaonya kwamba, itachukua miongo miwili kurekebisha nchi hiyo.