Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Tuesday, February 14, 2017

GAMBIA YATENGUA UAMUZI WA KUJIONDOA MAHAKAMA YA ICC

Gambia imetengua uamuzi wa kujiondoa katika Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC).
Masaa machache tu baada ya safari ya Boris Jonhnson, Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza nchini Gambia, viongozi wapya wa nchi hiyo wametangaza kuwa, nchi hiyo itaendelea kuwa mwanachama katika Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC).
Novemba mwaka jana aliyekuwa rais wa Gambia, Yahya Jammeh alitangaza habari ya kujiondoa nchi yake katika mahakama hiyo. Jammeh aliituhumu mahakama ya ICC kuwa inawaandama viongozi wa nchi za Kiafrika wakiwemo maafisa wa Gambia yenyewe.
Yahya Jammeh
Yahya Jammeh pia aliiondoa Gambia katika Jumuiya ya Madola, Commonwealth inayoongozwa na Uingereza na kutangaza kuwa, taasisi hiyo ni ukoloni mamboleo.
Rais mpya wa Gambia, Adama Barrow ambaye aliwahi kuwa mlinzi wa duka nchini Uingereza, ametangaza kuwa, ataimarisha uhusiano wa nchi hizo mbili na kwamba nchi hiyo itarejea tena katika Jumuiya ya Madola.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages