Tuesday, January 31, 2017

RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA MARAIS MBALIMBALI WA AFRIKA KATIKA MAKAO MAKUU YA UMOJA WA AFRIKA (AU) MJINI ADDIS ABABA ETHIOPIA

Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma akimkaribisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika moja ya Ofisi za Makao Makuu ya Umoja wa Afrika (AU) mjini Addis Ababa kwa ajili ya mazungumzo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma mara baada ya kuwasili kwa ajili ya mazungumzo katika Ofisi za Makao Makuu ya Umoja wa Afrika (AU) mjini Addis Ababa.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma mara baada ya kumaliza mazungumzo yao katika moja ya katika Ofisi za Makao Makuu ya Umoja wa Afrika (AU) mjini Addis Ababa nchini Ethiopia.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais wa Misri Abdel Fattah El Sisi kabla ya kuanza mazungumzo yao katika moja ya Ofisi za Makao Makuu ya Umoja wa Afrika (AU) mjini Addis Ababa nchini Ethiopia.
Rais wa Misri Abdel Fattah El Sisi akimkaribisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa ajili ya mazungumzo yao katika moja ya Ofisi za Makao Makuu ya Umoja wa Afrika (AU) mjini Addis Ababa nchini Ethiopia.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Rais wa Misri Abdel Fattah El Sisi mara baada ya kumaliza mazungumzo yao katika moja ya Ofisi za Makao Makuu ya Umoja wa Afrika (AU) mjini Addis Ababa nchini Ethiopia.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Rais wa Misri Abdel Fattah El Sisi mara baada ya kumaliza mazungumzo yao katika moja ya Ofisi za Makao Makuu ya Umoja wa Afrika (AU) mjini Addis Ababa nchini Ethiopia.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitoka kwenye mazungumzo yake pamoja na Rais wa Misri Abdel Fattah El Sisi
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Akinwumi Adesina mara baada ya kumaliza mazungumzo yao mjini Addis Ababa nchini Ethiopia.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni kabla ya kuanza mazungumzo yao katika moja ya Ofisi za AU mjini Addis Ababa Ethiopia.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni kabla ya kuanza mazungumzo yao rasmi katika moja ya Ofisi za AU mjini Addis Ababa Ethiopia.
. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Desalegn wakati akitoka kwenye mkutano wa AU mjini Addis Ababa nchini Ethiopia. 


PICHA NA IKULU

AU: AFRIKA IKO TAYARI KUPOKEA WAKIMBIZI BAADA YA USKUFUNGA MIPAKA YAKE

Umoja wa Afrika umesema nchi za Afrika ziko tayari kupokea wakimbizi baada ya Marekani kupasisha sheria tata ya kibaguzi dhidi ya wakimbizi.
Akizungumza pambizoni mwa mkutano wa AU unaomalizika leo mjini Addis Ababa, Ethiopia, Smail Chergui, Kamishna Mkuu wa Masuala ya Amani na Usalama wa Umoja wa Afrika amesema kuwa, bara la Afrika linafaa kuwa mfano mzuri wa kuigwa duniani kwa kuendelea kuwapokea wakimbizi na wahamiaji, baada ya Marekani kutangaza kuwa itafunga mipaka yake kuzuia wakimbizi na wahamiaji kuingia nchini humo.
Ameongeza kuwa, historia inaonyesha kuwa nchi za Kiafrika zimekuwa zikiwapokea wakimbizi kwa moyo mkunjufu huku akitoa mfano wa Kenya, ambayo ina kambi kubwa zaidi ya wakimbizi duniani ya Dadaab.
Wakimbizi wa Iraq
Chergui amesema vikosi vya kieneo vinapigana kufa kupona kuyatokomeza makundi ya kigaidi kama al-Shabaab na Boko Haram, hivyo haingii akilini Marekani kutangaza kuwafungia nje wakimbizi kwa kisingizio cha kupambana na ugaidi.
Smail Chergui, Kamishna Mkuu wa Masuala ya Amani na Usalama wa Umoja wa Afrika amesema kuwa, Marekani inafaa kutilia maanani wajibu wake wa kimataifa inapochukua uamuzi wowote wa kibaguzi na ambao unaweza kuhatarisha zaidi maisha ya wakimbizi.
Mwenyekiti anayeondoka wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika, Nkosazana Dlamini-Zuma hapo jana alikosoa mikakati ya kibaguzi inayochukuliwa na serikali ya Rais Donald Trump wa Marekani kwa kisingizio cha kupambana na ugaidi. 

Monday, January 30, 2017

CHINA: TAHADHARI YA KUTOKEA VITA NA MAREKANI SIO MANENO TU BALI NI KWELI HALISI

Viongozi wa China wamesema kuwa, indhari ya kutokea vita kati ya nchi hiyo na Marekani katika kipindi cha Rais Donald Trump, sio madai pekee, bali ni ukweli halisi.
Afisa mmoja wa ngazi ya juu katika jeshi la China ambaye hakutaka kutaja jina lake sambamba na kusema maneno hayo ameongeza kuwa, katika kujiandaa na vita na Marekani, jeshi la nchi hiyo limeweka mfumo wa ulinzi wa makombora katika bahari ya kusini na mashariki mwa China, kwa ajili ya ulinzi wa Peninsula ya Korea. Afisa huyo wa jeshi la China amesisitiza kuwa, Beijing imeingia katika awamu mpya ya kujiimarisha kiulinzi kutokana na hatari inayolikabili eneo la kusini mashariki mwa Asia.
Jeshi la Uchina
China imechukua hatua hizo kutokana na matamshi ya uhasama ya rais mpya wa Marekani Donald Trump dhidi ya nchi hiyo. Hivi karibuni pia jeshi la China lilitangaza kuwa, kuendelea kuwa mbaya hali ya mambo kuhusiana na usalama wa bahari ya eneo, machafuko katika eneo la Asia na Bahari ya Pasifiki na kadhalika misimamo tata ya rais huyo mpya wa Marekani, inailazimu kujiandaa kuingia katika vita tarajiwa na Marekani kuliko wakati mwingine wowote ule.
Jeshi la Uchina likiwa katika maandalizi
Ripoti hiyo ya jeshi la China ilifafanua kuwa, msimamo wa Washington wa kuweka ngao ya makombora ya THAD nchini Korea Kusini, kuongeza idadi ya askari wake katika maeneo ya mashariki na kusini mwa bahari za Uchina na kadhalika kuanzisha mlingano mpya wa kijeshi barani Asia, ni siasa ambazo zinaweza kuwasha moto wa vita wakati wowote. Mwezi Disemba mwaka jana, Donald Trump alitangaza kuwa, Washington haitafungamana na siasa za 'China Moja' kuhusiana na uhusiano wa nchi yake na Taiwan, suala ambalo lililalamikiwa na Beijing.
Makomando wa jeshi la China wakiwa katika mafunzo
Hii ni kwa kuwa mara kadhaa Beijing imekuwa ikitangaza kuwa, siasa za 'China Moja' ni suala lisilo na mjadala huku ikiitaka Washington kuangalia upya siasa zake kuhusiana na suala hilo.

JESHI LA YEMEN LAANGAMIZA MELI YA MIZIGO YA SAUDIA, RIYADH YAKIRI

Jeshi la Yemen Jumatatu ya jana liliangamiza meli ya mizinga ya Saudia na kusababisha makumi ya askari wa nchi hiyo vamizi kuangamizwa na wengine kujeruhiwa.
Sambamba na Saudia kukiri juu ya habari hiyo imedai kuwa, katika shambulizi la jeshi la Yemen dhidi ya meli yake ya mizinga katika pwani ya mkoa wa Al Hudaydah, askari wake wawili waliuawa na wengine watatu kujeruhiwa. Wakati huo huo jeshi la Saudia limeshambulia mji mdogo wa pwani wa Al Mukha kusini mwa mkoa wa Taiz na kusababisha makumi ya raia kuuawa shahidi na wengine wengi kujeruhiwa.
Mfalme wa Saudia anayetekeleza jinai na mauaji dhidi ya raia madhlumu wa Yemen
Aidha shambulizi hilo lilililenga daraja la Irfan mjini humo. Kwingineko jeshi la Yemen kwa kushirikiana na harakati ya wananchi ya Answarullah imeangamiza askari vibaraka wa Saudia waliokuwa wanakimbia uwanja wa mapigano baada ya kuzidiwa. Kwa mujibu wa habari hiyo askari kadhaa vibaraka wa Aal-Saud wameangamizwa katika mkoa wa Taiz kusini magharibi mwa Yemen.
Sehemu ya jinai za utawala wa kidikteta wa Aal-Saud huko Yemen
Hii ni katika hali ambayo kwa mara nyingine jeshi la Yemen limezilenga kambi za jeshi la Saudia za Jizan na kuisababisha nchi hiyo kibaraka wa Marekani na Israel hasara ya maafa na uharibifu. Kama ambavyo jeshi hilo la Yemen na harakati ya Answarullah limeshambulia kwa makombora mengi kambi ya jeshi ya al-Makhruq iliyopo eneo la Quwah mkoani Najran na kuangamiza askari kadhaa.

WATU WANANE WAUAWA KWA KUPIGWA RISASI MSIKITINI QUEBEC, CANADA

Quebec City
Polisi wamekiri kunao watu wamefariki lakini hawajataja idadi
Watu wanne wameuawa kwenye ufyatulianaji wa risasi katika msikiti mmoja mjini Quebec, Canada.
Ufyatulianaji wa risasi ulitokea katika Kituo cha Kitamaduni cha Kiislamu cha Quebec Jumapili usiku, polisi wamesema.
Kituo hicho kimepakia kwenye ukurasa wake wa Facebook video inayoonesha polisi wakiwa nje ya kitu hicho. Video hiyo imeambatana na ujumbe kwamba "baadhi wamefariki".
Polisi wamesema watu wawili wamekamatwa, lakini hawajatangaza idadi kamili ya waliofariki au kujeruhiwa.
Mtu aliyeshuhudia ameambia shirika la habari la Reuters kwamba watu hadi watatu waliokuwa na silaha wamehusika.
Shirika hilo la habari pia limesema maafisa wa usalama waliokuwa na silaha kali wameonekana wakiingia kwenye msikiti huo.
Gazeti la Le Soleil linasema limepata taarifa kwamba mmoja wa washukiwa ni kijana wa miaka 27 mwenye "jina la asili ya Quebec", na alikuwa na bunduki aina ya AK-47.
Ufyatuaji huo wa risasi umetokea katika msikiti ulio kwenye barabara ya Sainte-Foy, moja ya misikiti miwili inayoendeshwa na kituo hicho cha utamaduni wa Kiislamu.
Shambulio lilitekelezwa wakati wa sala ya jioni.
Polisi wamewakamata watu wawili
Polisi wamewakamata watu wawili
Rais wa msikiti huo Mohamed Yangui, ambaye hakuwa ndani ya msikiti wakati wa shambulio, ameambia Reuters kwamba hajafahamu kufikia sasa idadi ya waliojeruhiwa ingawa wamepelekwa hospitali mbalimbali Quebec.
"Nini kinatendeka hapa? Huu ni unyama," amesema.
Juni mwaka jana, kulipatikana karibu na mlango wa msikiti huo kichwa cha nguruwe kilichokuwa kimefungwa vizuri kama zawadi na kuandikwa "bonne appetit". Waislamu hawali nguruwe.
Kichwa
Kituo hicho kilisema zawadi hiyo ilikuwa "ishara ya chuki"
Waziri Mkuu wa Justin Trudeau ameandika kwenye Twitter kwa Kiingereza na Kifaransa na kusema, "Usiku huu, raia wa Canada wanaomboleza waliouawa kwenye shambulio hili la woga katika msikiti mmoja Quebec. Fikira zangu ni kwa waathiriwa na jamaa zao.

Thursday, January 26, 2017

RAIS BARROW AREJEA GAMBIA, ATAKA KIKAO CHA KIENEO KIBAKIE NCHINI MIEZI 6

Rais mpya wa Gambia Adama Barrow amerejea nchini kwake leo Alkhamisi akitokea nchi jirani ya Senegal, ambayo alilazimika kuigeuza kimbilio lake tangu Januari 15, akihofia usalama wake.
Mohammed Ibn Chambas, afisa wa Umoja wa Mataifa katika eneo la magharibi mwa Afrika amewaambia waandishi wa habari nchini Senegal kuwa, Barrow ameomba kikosi cha askari wa kieneo kisalie nchini humo kwa miezi sita zaidi, hadi mambo yatakapotengamaa. Afisa huyo wa UN ameongeza kuwa, uamuzi wa mwisho wa ombi la Rais Barrow utatolewa na Jumuiya ya Kiuchumi ya Magharibi mwa Afrika ECOWAS.
Rais Barrow akiapishwa katika ubalozi wa Gambia nchini Senegal wiki jana
Msemaji wa Barrow, Halifa Sallah amethibitisha kuwa, rais huyo mpya wa Senegal anaingia nchini leo na kwamba sherehe za kumpokea zitafanyika baadaye.
Rais Barrow anarejea Gambia baada ya kuondoka mtangulizi wake aliyeiongoza nchi hiyo ndogo ya magharibi mwa Afrika kwa miaka 22, Yahya Jammeh.
Jammeh ambaye yuko uhamishoni nchini Equatorial Guinea, anadaiwa kuondoka nchini Gambia na dola milioni 11 za Marekani kutoka hazina ya taifa, tuhuma ambazo kiongozi mpya wa taifa ameagiza zichunguzwe.
Yahya Jammeh akiondoka Banjul, Gambia
Wananchi wa Gambia wana matarajio mengi kutoka kwa uongozi wa Barrow. Tayari rais huyo mpya wa Gambia amemteua afisa wa zamani wa Umoja wa Mataifa, Fatoumata Tambajang kuwa makamu wake.

POLISI NIGERIA WAWAFYATULIA MABOMU YA KUTOWA MACHOZI WAFUASI WA SHEIKH ZAKZAKY

Maafisa usalama nchini Nigeria wamewafyatulia mabomu ya kutoa machozi wafuasi wa kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya nchi hiyo, Sheikh Ibrahim Zakzaky ambaye anaendelea kuzuiliwa kinyume cha sheria.
Shirika la habari la Press TV limeripoti kuwa, mamia ya wafuasi wa Sheikh Zakzaky hapo jana walifyatuliwa mabomu ya kutoa machozi walipokuwa wakishiriki maandamano ya amani ya kuonyesha uungaji mkono wao kwa kiongozi wao, nje ya bunge la nchi hiyo katika mji mkuu Abuja.
Maafisa wa polisi wa Nigeria waliyavunja maandamano hayo ya amani kwa mabomu ya machozi, ambapo watu kadhaa walijeruhiwa. Waandamanaji hao ambao walikuwa wamebeba picha za Zakzaky na maberamu yenye ujumbe unaosema, "Muachieni huru Zakzaky" walisikika wakiikosoa vikali serikali ya Abuja kwa kuendelea kumzuilia Sheikh Zakzaky licha ya agizo la mahakama.
Maandamano ya amani Abuja ya kushinikiza kuachiwa huru Sheikh Zakzaky
Itakumbukwa kuwa Mahakama ya Shirikisho la Nigeria hivi karibuni ilitoa amri ya kuachiliwa huru Sheikh Ibrahim Zakzaky, lakini serikali ya Rais Muhammadu Buhari wa nchi hiyo inavunja waziwazi amri hiyo ya mahakama kwa kukataa kumwachilia huru kiongozi huyo wa Harakati ya Kiislamu.
Umoja wa Ulaya na shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International ni baadhi ya taasisi za kimataifa zilizotoa taarifa zikiwataka viongozi wa Nigeria kuheshimu amri ya mahakama ya kumwachilia huru mara moja kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya nchi hiyo.

MEXICO: HATUTALIPIA UKUTA WA DONALD TRUMP

Rais Enrique Pena Nieto wa Mexico kushoto na mwenzake wa Marekani Donald Trump kulia
Rais Enrique Pena Nieto wa Mexico kushoto na mwenzake wa Marekani Donald Trump kulia
Mexico imesema kuwa haitalipia ukuta uliopendekezwa na rais wa Marekani Donald Trump ,kulingana na rais wa taifa hilo Enrique Pena Nieto ambaye ameshutumu mpango huo wa kujenga ukuta.
Hata hivyo rais huyo hakizungumzia kuhusu iwapo atafutilia mbali ziara yake ya Marekani ambapo anatarajiwa kukutana na rais Donald Trump.
Trump tayari amesaini agizo la urais la kujenga ukuta kati ya Marekani na Mexico na amesisitiza kuwa Mexico itailipa Marekani kwa ukuta huo.
Rais Pena Nieto aliambia taifa katika hotuba ya runinga kwamba :Nimesema tena na tena kwamba Mexico haitalipia ukuta huo.
''Ninajuta na kushutumu uamuzi huo wa marekani wa kutaka kuendelea kujenga ukuta ambao umetugawanya kwa miaka badala ya kutuunganisha''.
Lakini Nieto amesema kuwa urafiki kati ya Mexico na raia wa Marekani utadumu mbali na kutafuta suluhu kuhusu tatizo la wahamiaji.
Waziri wa maswala ya kigeni nchini Mexico Luis Videgaray ambaye yuko mjini Washington amesema kuwa rais huyo bado anaendelea kupima uwezekano wa ziara ya Marekani siku ya Jumanne lakini akaongezea kuwa mkutano huo bado utafanyika kufikia sasa.

Wednesday, January 25, 2017

WASOMALI 90 NA WAKENYA WAWILI WATIMULIWA MAREKANI

Raia takriban 90 wa Somalia na wawili wa Kenya wametimuliwa kutoka Marekani saa chache baada ya taarifa kuibuka kwamba Rais Donald Trump atakabiliana na watu wanaoishi nchini humo kinyume cha sheria.
Wote waliwasili katika uwanja wa kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi, lakini baadaye raia wa Somalia wakaendelea na safari hadi uwanja wa ndege wa Aden Abdulle mjini Mogadishu. Msemaji wa serikali ya Kenya Eric Kiraithe ameambia BBC kwamba ni kweli raia hao wamefukuzwa Marekani, ingawa hakusema iwapo hatua hiyo imetokana na msimamo wa Bw Trump.. "Ni watu 90 kulingana na habari ambazo tulipewa. Wakati unaondolewa nchi fulani kurejeshwa kwenu, huwa unarejeshwa hadi kwenu," ameambia BBC. Kuhusu sababu iliyowafanya kufurushwa, Bw Kiraithe amesema: "Inategemea sheria za nchi ambayo walikuwa wamehamia (Marekani),"

Monday, January 23, 2017

GARI LA KIFAHARI LA RAIS JAMMEH ALIYEKIMBIA NCHI BALAA..ANADAIWA KUKOMBA PESA KATIKA HAZINA YA NCHI YA GAMBIA

Yahya Jammeh aliyeitawala Gambia kwa miaka 22, hatimaye jana aliondoka nchini humo na kwenda kuishi uhamishoni baada ya kushindwa katika uchaguzi mkuu wa Disemba Mosi mwaka jana.Jammeh alishindwa na kiongozi aliyekuwa akiungwa mkono na vyama vya upinzani, Adama Barrow ambaye amekuwa akiishi nchni Senegal alipoapishwa kuwa Rais wa Gambia baada ya Jammeh kukataa kutoka madarakani awali. Yahya Jammeh alipokuwa akiiongoza Gambia aliweza kujinunulia vitu vingi vya kifahari na moja wapo ni gari lake la kifahari aina ya Rolls Royce.
Gari hili ambalo kwenye viti vyake ameandika jina lake, lina thamani ya kati ya fedha za kitanzania milioni 500 hadi milioni 800. Rolls Royce ni moja ya magari ya kifahari na ya kipekee duniani ambayo mara nyingi hutumiwa na watu wenye uwezo mkubwa kifedha.
Gari hili la Yahya Jammeh liliwashangaza rais wengi wa Gambia lilipokuwa likikatisha katika viunga vya mji wa Banjul kumpeleka kiongozi huyo uwanja wa ndege tayari kuondoka nchini humo.
Licha ya kuwa Jammeh aliondoka nchini Gambia jana huku wananchi wakishangilia kwa furaha, imeelezwa kuwa kiongozi huyo alikomba fedha katika hazina ya nchini hiyo na kuiacha katika ukata mkubwa wa fedha.Taarifa kutoka katika kambi ya Rais Adama Barrow zinaeleza kuwa dola za kimarekani milioni 11 zilichukuliwa katika hazina ya nchi hiyo.Yahya Jammeh tayari amewasili nchini Equatorial Guinea ambapo ndipo ataishi.
Hapa chini ni picha zaidi za gari hilo la kifahari;
Hapa ni sehemu ya magari ya Yahya Jammeh yalipo uwanja wa ndege wa Banjul Gambia, baada ya ndege toka Guinea kuzuiliwa kuyachukua.

WATU ZAIDI YA 19 WAPOTEZA MAISHA BAADA YA JIMBO LA GEORGIA KUKUMBWA NA KIMBUNGA, RAIS TRUMP ATUMA SALAM ZA RAMBIRAMBI

Image result for tornado HIT GEORGIA JAN 22, 2017
Wakazi wa mji wa Albany jimbo la Georgia wakiwa na hudhuni kubwa baada ya nyumba zao kubomolewa na kimbunga siku ya Jumapili Jan 22, 2017 na inasadikika watu zaidi ya 19 wamepoteza maisha na zaidi ya watu 23, wamejeruhiwa. Rais Donald Trump aliongea kwa simu ya Gavana wa jimbo hilo na kutuma salam za rambirambi na kutoa pole kwa wananchi wa jimbo hilo kwa kukumbwa na kimbunga hicho kilichoikumba mji huo kusini ya jimbo la Georgia inayopakana na sehemu ya kaskazini ya jimbo la Florida.
Image result for tornado HIT GEORGIA JAN 22, 2017
Sehemu iliyoharibiwa na kimbunga hicho.
Image result for tornado HIT GEORGIA JAN 22, 2017
Mmoja ya waathirika wa kimbunga akiwa kwenye majonzi mengi.

Image result for tornado HIT GEORGIA JAN 22, 2017
Nyumba ikiwa imeharibiwa vibaya na kimbunga.
Image result for tornado HIT GEORGIA JAN 22, 2017
Miti ikiwa imeanguka na paa likiwa limeuzuliwa na kimbunga kilichoikumba jimbo la Georgia.

Friday, January 20, 2017

BARROW: YAHYA JAMMEH AMEKUBALI KUONDOKA MADARAKANI GAMBIA

Rais Yahya Jammeh wa Gambia amekubali kuondoka madarakani kumpisha rais mpya Adama Barrow.
Kwa mujibu wa ripoti,  Jammeh anaondoka nchini humo kwenda kuishi uhamishoni, ingawa bado haijafahamika ni nchi gani ataelekea. Habari za kuondoka rais huyo aliyetawala Gambia kwa miaka 22 sasa zimetolewa na rais anayetambuliwa na jamii ya kimataifa Adama Barrow kupitia mtandao wake wa Twitter. Barrow ameeleza hayo baada ya mazungumzo ya saa kadha yaliyokusudia kumshawishi Yahya Jammeh kukubali matokeo ya uchaguzi wa tarehe Mosi Disemba mwaka jana.
Aliyekuwa rais wa Gambia Yahya Jammeh
Hii ni katika hali ambayo nchi kadhaa za Afrika Magharibi zimewatuma wanajeshi wao nchini Gambia na kutishia kumuondoa Jammeh madarakani kwa nguvu iwapo angekaidi amri ya kuachia madaraka kwa hiari. Barrow amekuwa nchini Senegal kwa takriban wiki moja sasa ambapo pia aliapishwa kuwa rais mpya wa Gambia katika ubalozi wa nchi hiyo mjini Dakar Alkhamisi iliyopita. Sasa Barrow anatambuliwa na jamii ya kimataifa kuwa kiongozi mpya wa Gambia.