Serikali ya Rwanda imewafukuza kazi maafisa
polisi 200 waliohusishwa na ufisadi nchini humo. Uchunguzi wa hivi
karibuni uliofanywa na Taasisi ya Transparency International umeonyesha
kuwa Rwanda ni nchi ya tatu yenye ufisadi wa kiwango cha chini katika
nchi za chini ya Jangwa la Sahara barani Afrika.
Bi
Marie- Imamaculate Ingabire Mkuu wa Taasisi ya Transparencyy
International nchini Rwanda amesema kuwa kuorodheshwa Rwanda kuwa nchi
yenye ufisadi wa kiwango cha chini kunadhihirisha azma iliyonayo
serikali katika kukomesha ufisadi nchini humo. Serikali ya Rwanda
iliidhinisha kufukuzwa maafisa hao wa polisi katika mkutano wake wa
Ijumaa iliyopita chini ya uwenyekiti wa Rais Paul Kagame. Serikali ya
Rwanda imekuwa ikipongezwa na nchi wafadhili kwa hatua yake ya
kuwaadhibu maafisa mafisadi. Naye Msemaji wa jeshi la polisi la Rwanda
Theos Badege amesema kuwa hakuna kuonewa huruma wala kupewa msamaha
maafisa polisi wanaohusika na ufisadi. Amesema ni sera ya taifa
kuhakikisha kwamba vitendo vyote vya ufisadi vinakabiliwa na mkono wa
sheria.
Raia 200 walitiwa mbaroni mwaka jana huko Rwanda wakituhumiwa kutoa rushwa kwa polisi.
No comments:
Post a Comment