Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Wednesday, February 15, 2017

KIONGOZI MUADHAMU: VITISHO VYA VITA VYA KIJESHI, NI HILA ZILIZOZOELEKA ZA MAREKANI

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza kuwa, Marekani inatumia hila ya kurudia rudia vitisho vya kuishambulia kijeshi Iran ili kuwatoa viongozi wa Jamhuri ya Kiislamu katika uwanja wa vita vya kweli ambavyo ni vita vya kiuchumi.
Ayatullahil Udhma Sayyid Ali Khamenei amesema hayo leo wakati alipoonana na maelfu ya wananchi wa Azerbaijan (kaskazini magharibi mwa Iran) na kusema kuwa, kujitokeza kwa wingi, kwa moyo mmoja na kwa hamasa kubwa wananchi wa Iran katika matembezi ya Bahman 22 ya kuadhimisha ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ni jambo lililoyaletea fakhari kubwa mapinduzi hayo na mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu humu nchini. 
Aidha amewashukuru wananchi wote wa Iran kwa kuwaambia: Mwaka huu si vyombo vya habari vya ndani pekee vilivyoripoti kushiriki kwa wingi sana wananchi wa Iran kwenye matembezi hayo, bali hata maadui wa Mapinduzi ya Kiislamu nao - tofauti na miaka ya huko nyuma - mwaka huu wamekiri kuwa mamilioni ya wananchi wa Iran wameshiriki kwenye maadhimisho hayo.
Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ametoa uchambuzi kuhusu lengo hasa la serikali iliyopita na ya hivi sasa ya Marekani la kutoa vitisho vya mara kwa mara vya kuishambulia kijeshi Iran na kuongeza kuwa: Kama walivyofanya huko nyuma, leo hii pia wanatoa matamshi hayo hayo ya kwamba chaguo la mashambulizi ya kijeshi dhidi ya Iran liko mezani. Na yule afisa wa barani Ulaya naye aliyewaambia viongozi wa Iran kuwa, "kama si makubaliano ya nyuklia ya JCPOA, basi vita dhidi ya Iran lilikuwa ni jambo lisiloepukika" lakini matamshi hayo ni uongo ulio wazi. Wanataka kuzibabaisha akili zetu na kutufanya tusahau vita vya kweli, yaani vita vya kiuchumi. Wanajaribu kuzivuta fikra zetu upande wa vita vya kijeshi ili viongozi wa nchi yetu wasahau kuelekeza nguvu zao upande wa maendeleo ya kiuchumi na vita vya kiutamaduni vya Wamagharibi dhidi ya taifa la Iran.

Aidha ameashiria jinsi mashirika ya kijasusi ya Marekani CIA na utawala wa Kizayuni wa Israel MOSSAD pamoja na mashirika ya kijasusi ya Uingereza na fedha za mafuta za watawala "Maqarun" zinavyotumika kuandaa mazingira mabaya na kuendesha propaganda chafu dhidi ya Mapinduzi na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kusema: Katika kipindi cha miaka yote hii, mamia ya kanali za televisheni na mitandao ya kijamii ya maadui wa Mapinduzi ya Kiislamu imekuwa ikifanya njama za kuidunisha na kuidhoofisha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Hata hivyo kujitokeza kwa wingi wananchi wa Iran katika matembezi ya Bahman 22 ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu huondoa vumbi lililopandikizwa na maadui hao na kuyasafisha Mapinduzi na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
 Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu pia amesema, maendeleo iliyopiga Iran kwenye kipindi cha miongo minne iliyopita katika masuala ya miundombinu ni ya kustaajabisha. Amesema: Baadhi ya maendeleo hayo kikawaida yasingeliweza kufikiwa hata baada ya kupita miaka mia moja.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages