Mahakama ya rufaa ya Marekani imepinga amri ya Rais
Donald Trump iliyopiga marufuku wahamiaji wa nchi saba za Kiislamu
kuingia nchini humo. Trump pia ameukubali msimamo wa China wa kuitaja
Taiwan kuwa ni sehemu yake
Muda mfupi baada ya mahakana kutoa uamuzi wake, Trump aliandika
katika ukurasa wake wa Twitter kwa kutumia herufi kubwa, "TUTAKUTANA
MAHAKAMANI," na kuongeza "USALAMA WA NCHI YETU UKO HATARINI!"
Na
akajibiwa na Jay Inslee, Gavana wa Washington mwanachama wa chama cha
Democratic anayeongoza moja ya majimbo yaliyopinga marufuku hiyo. Inslee
ameandika "Bwana Rais, tumeshakutana mahakamani, na tumekushinda!"
Waislam nchini Marekani wamefurahishwa na hukumu hiyo ya mahakama ya rufaa.
"Leo
ni siku kubwa kwa demokrasia. Mahakama imetuma ujumbe mzito sana kwamba
hakuna mtu, pamoja na rais wa Marekani, aliye juu ya sheria. Kimsingi
mahakama imesema, katika kukabiliana na hoja ya serikali ya Marekani,
kwamba hata rais, matendo yake lazima yapitiwe na mahakama ya
shirikisho, hasa pale kunapoulizwa maswali iwapo matendo ya rais
yanakiuka Katiba," Farhana Khera, mkurugenzi mtendaji wa umoja wa
mawakili wa Kiislam, wa shirika la kulinda haki za kiraia za Waislam wa
Marekani.
Maamuzi ya rais lazima yapitiwe na mahakama
Majaji
hao pia wamepinga hoja ya uongozi wa Trump kwamba mahakama hazina
mamlaka ya kupitia maamuzi ya rais yanayohusu uhamiaji na usalama wa
taifa.
Wamesema kwamba serikali imeshindwa kuthibitisha kwamba
amri hiyo imetimiza vigezo vya kikatiba vya kutoa ilani au kuwasilisha
pendekezo la amri hiyo likasikilizwa mahakamani kabla ya kupiga marufuku
ya kusafiri.
Majaji hao pia wamesema uongozi wa Trump umeshindwa
kuwasilisha ushahidi kwamba kuna mgeni yeyote kutoka nchi hizo saba
aliyehusika na shambulio la kigaidi nchini Marekani.
Rais wa China Xi Jinping (kushoto) na Rais wa Marekani Donald Trump (kulia)
Kwa
sasa, ina maana wahamiaji na raia kutoka nchi hizo saba zilizo na
Waislamu wengi zilizotajwa katika amri ya rais Trump ya kushtukizia,
wataendeleo kuingia nchini humo.
Wasafiri hao hawatokamatwa
wakiwasili Marekani, hawatorudishwa walipotokea, na pia maandamano
yanayopinga amri ya Trump na yaliyokuwa yamejaza watu ndani ya viwanja
vya ndege nchini humo yatamalizika.
Trump aunga mkno sera ya "China moja"
Na
kuhusu mahusiano kati ya China na Marekani, msemaji wa Ikulu ya White
House amesema, Trump alifanya mazungumzo marefu na Rais wa China Xi
Jinping kwa njia ya simu jana usiku, na kwamba Marekani imekubali
kuheshimu sera ya China ya kile inachokiita "China moja." Kwa maana hiyo
Marekani imekubali msimamo wa China kwamba kuna China moja tu na Taiwan
ni sehemu yake.
Wakati huo huo, baraza la Seneti la Marekani
limemuidhinisha, Tom Price, kuwa Waziri wa Afya. Kura 52 zilimuunga
mkono na 47 zilimpinga.
No comments:
Post a Comment