Russia imesema haikubaliani na mtazamo wa serikali ya Rais Donald Trump wa Marekani wa kuielezea Iran kuwa ni "dola la kigaidi".
Akizungumza na kanali ya televisheni ya Fox News hapo jana, Trump alidai kuwa Iran ni "dola nambari moja la kigaidi".
Matamshi
ya rais wa Marekani yanafanana na madai yaliyotolewa siku ya Jumamosi na
Waziri wake wa Ulinzi James Mattis ambaye alisema Iran ni "dola
mfadhili mkubwa zaidi wa ugaidi duniani".
Akijibu matamshi hayo, msemaji wa Ikulu ya Russia, Kremlin, Dmitry Peskov amesema: "Hatukubaliani na dhana hii".
Peskov
ameashiria ushirikiano na uitifaki uliopo baina na Tehran na Moscow
katika masuala mbalimbali na kusisitiza kuwa Russia inakusudia
kustawisha uhusiano wake na Iran.
"Nyote
mnajua kwamba Russia ina uhusiano mzuri wa uitifaki na Iran, na
tunashirikiana na nchi hiyo katika mambo kadhaa. Tunathamini uhusiano
wetu katika uga wa biashara na uchumi na tuna matumaini ya kuustawisha
zaidi uhusiano huo", amesisitiza afisa huyo wa Russia.
Hii ni katika hali ambayo viongozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran
wamekanusha tuhuma za kufadhili ugaidi zinazotolewa na serikali ya
Marekani na kusisitiza kwamba Tehran iko mstari wa mbele katika vita
dhidi ya ugaidi.
Iran
imekuwa ikitoa msaada wa ushauri wa kijeshi kwa nchi za Iraq na Syria
katika vita vyao dhidi ya ugaidi. Aidha imekuwa ikishirikiana na Russia
kuisaidia kijeshi serikali ya Syria katika vita hivyo…
No comments:
Post a Comment