Uganda imeomba kupewa msaada wa kimataifa kwa ajili ya kutatua mgogoro wa wakimbizi wamaomiminika nchini humo.
Waziri wa Misaada, Kukabiliana na Majanga na Wakimbizi wa
Uganda, Hillary Onek amesema kuwa, usimamizi wa masuala ya wakimbizi
umekuwa mgumu zaidi kutokana na idadi kubwa ya wakimbizi wanaoingia
nchini humo.
Waziri Hillary Onek ameongeza kuwa, Uganda inakabiliwa na ongezeko kubwa la wakimbizi.
Uganda imewapa hifadhi wakimbizi zaidi ya milioni moja, nusu yao
wakiwa ni kutoka nchi jirani ya Sudan Kusini ambako mapigano ya ndani
bado yanaendelea. Kwa wastani wakimbizi 4,000 wa Sudan Kusini
wanasemekana kuvuka mpaka kila siku na kuingia Uganda.
Wakimbizi wengine walioko Uganda ni kutoka nchi za Rwanda, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Burundi, Eritrea na Ethiopia.
Uganda imesifiwa kimataifa kutokana na sera yake ya kufungua
milango kwa wakimbizi wakati nchi nyingi zimefunga milango yao mbele ya
wakimbizi wanaokimbia nchi zao kwa ajili ya kuokoa maisha.
No comments:
Post a Comment