Wakazi wa mji wa Albany jimbo la Georgia wakiwa na hudhuni kubwa
baada ya nyumba zao kubomolewa na kimbunga siku ya Jumapili Jan 22, 2017
na inasadikika watu zaidi ya 19 wamepoteza maisha na zaidi ya watu 23,
wamejeruhiwa. Rais Donald Trump aliongea kwa simu ya Gavana wa jimbo
hilo na kutuma salam za rambirambi na kutoa pole kwa wananchi wa jimbo
hilo kwa kukumbwa na kimbunga hicho kilichoikumba mji huo kusini ya
jimbo la Georgia inayopakana na sehemu ya kaskazini ya jimbo la Florida.
Sehemu iliyoharibiwa na kimbunga hicho.
Mmoja ya waathirika wa kimbunga akiwa kwenye majonzi mengi.
Nyumba ikiwa imeharibiwa vibaya na kimbunga.
Miti ikiwa imeanguka na paa likiwa limeuzuliwa na kimbunga kilichoikumba jimbo la Georgia.
No comments:
Post a Comment