Maeneo mengi ya bara la Afrika mwaka huu mpya
wa 2017 yataendelea kusumbuliwa na uhaba wa chakula na hatari ya baa la
njaa na ukame kwa kadiri kwamba, Umoja wa Mataifa umeeleza wasiwasi
kwamba karibu watu milioni 20 hawatakuwa na usalama wa chakula katika
nchi za kaskazini na mashariki mwa Afrika.
Taasisi za misaada ya kibinadamu za Umoja wa Mataifa
zimetangaza kuwa, karibu watu milioni 20 katika nchi za Afrika
wanahitajia misaada ya dharura ya chakula na kwamba hakuna matarajio
kuwa mahitaji hayo yatakidhiwa katika miezi kadhaa ijayo.
Ripoti iliyotolewa na Idara ya Uratibu wa Misaada ya Kibinadamu ya
Umoja wa Mataifa kuhusu athari mbaya mvua kali katika maeneo ya
kaskazini na mashariki mwa Afrika inasema kuwa, mavuno yasiyokuwa mazuri
ya mazao ya kilimo katika miezi ya Aprili na Mei mwaka huu yataboresha
kwa muda hali ya upatikanaji wa chakula katika maeneo hayo ya Afrika
lakini kwa mujibu wa tathmini na makadirio ya kitaalamu, uhaba wa
chakula katika nchi za Afrika katika kipindi cha kuanzia mwezi Julai
utashadidi tena na wakazi wa nchi hizo watakabiliwa na hali mbaya ya
ukosefu wa chakula.
Mvua kali zilizonyesha katika eneo la mashariki mwa Afrika mwishoni
mwa mwezi Aprili zimesababisha mafuriko makubwa na kuathiri maisha ya
zaidi ya watu nusu milioni wa eneo hilo. Ripoti ya Idara ya Uratibu wa
Misaada ya Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa inasema kuwa, mvua hizo
zimeboresha kiasi hali ya mambo kwa muda katika maeneo kama Ethiopia na
Somalia ambayo yameathiriwa na ukame mkali na wa muda mrefu wa miongo
kadhaa iliyopita lakini hali hiyo haitaendelea kwa kipindi kirefu na
wala haitakuwa na taathira katika kuondoa athari mbaya za ukame mkubwa
uliosababishwa na majanga ya kimaumbe kama yale ya El Nino.
Mabadiliko ya hali ya hewa, vita, machafuko ya ndani na kuongezeka
harakati za kigaidi vimeziathiri zaidi nchi za Afrika. Kwa sasa nchi
kama Ethiopia, Zimbabwe, Somalia, Jamhuri ya Afrika ya Kati na Sudan
Kusini zinasumbuliwa na uhaba wa chakula. Machafuko na mivutano ya
kisiasa katika baadhi ya nchi za Kiafrika na vilevile kupungua kwa pato
la serikali vimezidisha umaskini na hali mbaya ya kimaisha. Haya yote
yanatokea sambamba na nchi za Magharibi zinazodai kujali ubinadamu
zikikataa kutimiza ahadi zao na kutoa fungu la misaada ya kifedha kwa
taasisi za kimataifa za misaada ya kibinadamu ambazo sasa zinazumbuliwa
na uhaba wa fedha kwa ajili ya kudhamini chakula, dawa na mahitaji
mengine ya kimsingi ya wanadamu wanaosumbuliwa na matatizo ya aina
mbalimbali.
Mwaka uliopita viongozi na wawakilishi wa nchi mbalimbali duniani
walioshiriki katika mkutano wa Paris, Ufaransa walichukua jukumu la
kupunguza athari mbaya za mabadiliko ya hali ya hewa kupitia njia ya
kufanyia mabadiliko sera na siasa zao na kutoa misaada zaidi kwa nchi
zilizoathiriwa na hali hiyo. Hata hivyo kuna hatari kwamba nchi nyingi
kubwa zilizoshiriki katika mkutano huo hazitatekeleza ahadi na
makubaliano ya Paris. Kwa mfano tu rais mteule wa Marekani, Donald Trump
ametangaza kuwa hataheshimu makubaliano ya hali ya hewa ya Paris.
Kwa msingi huo inazatamiwa kuwa, nchi nyingi za ulimwengu wa tatu
hususan zile za Afrika zitakabiliwa na hali mbaya ya umaskini na njaa
katika mwaka huu mpya na hata maafa makubwa ya kibinadamu iwapo jamii ya
kimataifa haitachukua hatua za maana za kudhamini mahitaji ya njaa
No comments:
Post a Comment