Polisi wamekiri kunao watu wamefariki lakini hawajataja idadi
Watu wanne wameuawa kwenye ufyatulianaji wa risasi katika msikiti mmoja mjini Quebec, Canada.
Ufyatulianaji wa risasi ulitokea katika Kituo cha Kitamaduni cha Kiislamu cha Quebec Jumapili usiku, polisi wamesema.
Kituo
hicho kimepakia kwenye ukurasa wake wa Facebook video inayoonesha polisi
wakiwa nje ya kitu hicho. Video hiyo imeambatana na ujumbe kwamba
"baadhi wamefariki".
Polisi wamesema watu wawili wamekamatwa, lakini hawajatangaza idadi kamili ya waliofariki au kujeruhiwa.
Mtu aliyeshuhudia ameambia shirika la habari la Reuters kwamba watu hadi watatu waliokuwa na silaha wamehusika.
Shirika hilo la habari pia limesema maafisa wa usalama waliokuwa na silaha kali wameonekana wakiingia kwenye msikiti huo.
Gazeti la
Le Soleil linasema limepata taarifa kwamba mmoja wa washukiwa ni kijana
wa miaka 27 mwenye "jina la asili ya Quebec", na alikuwa na bunduki
aina ya AK-47.
Ufyatuaji
huo wa risasi umetokea katika msikiti ulio kwenye barabara ya
Sainte-Foy, moja ya misikiti miwili inayoendeshwa na kituo hicho cha
utamaduni wa Kiislamu.
Shambulio lilitekelezwa wakati wa sala ya jioni.
Polisi wamewakamata watu wawili
Rais wa
msikiti huo Mohamed Yangui, ambaye hakuwa ndani ya msikiti wakati wa
shambulio, ameambia Reuters kwamba hajafahamu kufikia sasa idadi ya
waliojeruhiwa ingawa wamepelekwa hospitali mbalimbali Quebec.
"Nini kinatendeka hapa? Huu ni unyama," amesema.
Juni
mwaka jana, kulipatikana karibu na mlango wa msikiti huo kichwa cha
nguruwe kilichokuwa kimefungwa vizuri kama zawadi na kuandikwa "bonne
appetit". Waislamu hawali nguruwe.
Kituo hicho kilisema zawadi hiyo ilikuwa "ishara ya chuki"
Waziri
Mkuu wa Justin Trudeau ameandika kwenye Twitter kwa Kiingereza na
Kifaransa na kusema, "Usiku huu, raia wa Canada wanaomboleza waliouawa
kwenye shambulio hili la woga katika msikiti mmoja Quebec. Fikira zangu
ni kwa waathiriwa na jamaa zao.
No comments:
Post a Comment