Akbar Hashemi Rafsanjani
Kiongozi
wa kidini wa Iran, Ayatollah Ali Khamenei, ameongoza kutoa salamu za
rambirambi za kifo cha aliyekuwa rais wa nchi hiyo, Akbar Hashemi
Rafsanjani, aliyefariki dunia, akiwa na umri wa miaka themanini na
mbili.
Licha ya tofauti walizokuwa nazo viongozi hao, lakini kiongozi huyo wa dini amemtaja Rafsanjani kama mpambanaji.
Rafsanjani alikuwa akimuunga mkono rais wa sasa Hassan Rouhani ambae amemsifu kuwa ni mwana mapinduzi mkubwa.
Siku tatu za maombolezi zimetangazwa.
Ayatollah Rafsanjani aliwahi kuwa rais kati ya mwaka 1989 hadi 1997 na ameendelea kuwa na nafasi muhimu katika siasa za Iran
No comments:
Post a Comment