Jeshi la Syria limetangaza kuwa utawala wa
kizayuni wa Israel umeshambulia uwanja wa ndege wa kijeshi wa Mezzah
ulioko magharibi mwa mji wa Damascus na kuutahadharisha utawala huo
kuhusu taathira mbaya za shambulizi hilo.
Taarifa
ya jeshi la Syria imesema uwanja huo wa ndege wa kijeshi umeshambuliwa
kwa maroketi kadhaa usiku wa kuamkia leo na kusisitiza kwamba, Syria
italipiza kisasi shambulizi hilo.
Taarifa
hiyo imesema, shambulizi la Israel dhidi ya uwanja wa ndege wa kijeshi
wa Mezzah ni jaribio la utawala huo ghasibu la kutaka kuyasaidia makundi
ya kigaidi yanayoelekea kusambaratika na kwamba Damascus itaendeleza
mapambano na vita hadi ugaidi utakapotokomezwa kikamilifu nchini humo.
Ripoti zinasema shambulizi hilo la Israel lililenga maghala ya mafuta
yanayotumiwa na kikosi maalumu cha jeshi la Syria cha Republican
Guards.
Israel
inahesabiwa kuwa miongoni mwa pande zinazoyasaidia na kuyaunga mkono
makundi ya kigaidi nchini Syria hususan kundi la magaidi wa Daesh.
No comments:
Post a Comment