Karibu walowezi 50 wa Kizayuni leo Alkhamisi
wamekivamia tena Kibla cha Kwanza cha Waislamu yaani Masjidul Aqswa na
kuuvujia heshima msikiti huo mtakatifu kwa ulinzi kamili wa polisi wa
Israel.
Kituo cha Upashaji Habari cha
Palestina kimeripoti habari hiyo na kuongeza kuwa, walowezi Wazayuni
wameuvamia Msikiti wa al Aqsa kwa mara kadhaa katika kipindi cha wiki
moja iliyopita na kuwashambulia walinzi wa eneo hilo takatifu.
Kwa mujibu wa kituo hicho cha habari,
vitendo vya walowezi wa Kizayuni vya kuvamia Kibla cha Kwanza cha
Waislamu vinazidi kuongezeka.
Mwezi Machi mwaka huu. walowezi 1,782 wa
Kizayuni waliuvamia Msikiti wa al Aqsa na kuuvunjia heshima msikiti huo
mtakatifu ikiwa ni ongezeko la takriban mara mbili ikilinganishwa na
mwezi Machi mwaka jana ambapo walowezi 960 walilivamia eneo hilo tukufu.
Mwezi Machi mwaka huu pia, taasisi zenye
misimamo mikali za Kiyahudi zilitoa mwito mara kadhaa wa kuvamiwa na
Wazayuni, Kibla cha Kwanza cha Waislamu.
Masjidul Aqswa imegeuzwa kuwa eneo la
kuonesha jeuri za wanajeshi wa Israel na walowezi wa Kizayuni wenye nia
ya kuupokonya msikiti huo sura na utambulisho wake wa Kiislamu.
Kuwepo msikiti huo mtakatifu na maeneo
mengine matukufu kwa Waislamu na Wakristo, kunaufanya mji wa Baytul
Muqaddas huko Palestina kuwa eneo takatifu kwa wafuasi wa dini hizo
mbili.
Hata hivyo utawala wa Kizayuni wa Israel
unafanya njama za kila namna za kuuyahudisha mji huo na kuupokonya
kabisa sura yake ya Kiislamu na pia ya Kikristo.
No comments:
Post a Comment