Idadi ya Wajerumani waliojitokeza kupiga kura katika uchaguzi wa
jimbo dogo la magharibi la Saarland ni juu kidogo kuliko idadi ya
waliojitokeza katika uchaguzi uliopita wa mwaka 2012. Hadi kufikia saa
nane mchana wa leo takriban asilimia 32.6 ya wapiga kura walishapiga
kura zao, tofauti na uchaguzi uliopita ambapo wakati sawa na huo, ni
asilimia 31.1 ya wapiga kura ndio walikuwa wamejitokeza. Ongezeko la
asilimia hiyo ndogo inatizamwa kuwa ishara za awali ya jinsi hali
itakavyokuwa katika uchaguzi mkuu wa Ujerumani mwezi Septemba. Uchaguzi
huo unaojiri miezi sita kabla ya uchaguzi mkuu mwezi Septemba,
unatizamwa kama kipimo kinachoweza kubaini ushawishi wa Kansela Angela
Merkel dhidi ya washindani wake wa siasa za wastani za mrengo wa
kushoto. Uchaguzi huo ni wa kwanza miongoni mwa chaguzi tatu za majimbo
zitakazofanyika kabla ya uchaguzi mkuu. Kadhalika ndio uchaguzi wa
kwanza tangu Martin Schulz kuidhinishwa na chama chake cha SPD kugombea
ukansela dhidi ya Merkel.
Post Top Ad
Your Ad Spot
Sunday, March 26, 2017
Home
Unlabelled
WENGI WAJITOKEZA KATIKA UCHAGUZI WA SAARLAND UJERUMANI KULIKO 2012
WENGI WAJITOKEZA KATIKA UCHAGUZI WA SAARLAND UJERUMANI KULIKO 2012
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
Author Details
Ut wisi enim ad minim veniam, quis nostrud exerci tation ullamcorper suscipit lobortis nisl ut aliquip ex ea commodo consequat. Duis autem vel eum iriure dolor in hendrerit in vulputate velit esse molestie consequat.
No comments:
Post a Comment