Jeshi la Nigeria limetangaza kuwa limetuma
askari 200 na ndege kadhaa za kivita katika nchi jirani na Gambia ya
Senegal kwa ajili ya kutatua mgogorowa uongozi uliosababishwa na
uchaguzi wa rais nchini Gambia.
Taarifa iliyotolewa na Jeshi la Anga la Nigeria imesema kuwa,
kundi la askari 200, ndege kadhaa za kivita, manuari ya kijeshi,
helikopta na ndege za ujasusi zimepelekwa nchini Senegal kwa ajili ya
kufuatilia hali ya mambo nchinI Gambia.
Hatua hiyo imechukuliwa huku nchi za Magharibi mwa Afrika
zikijitayarisha kutuma majeshi nchini Gambia kwa ajili ya kumuondoa
madarakani kwa nguvu Bwana Yahya Jammeh ambaye kipindi chake cha uongozi
kinamalizika leo.
Senegal pia imetangaza kuwa iwapo Yahya Jammeh atang'ang'ang'ania
madaraka jeshi la nchi hiyo liko tayari kuingia nchini humo na kurejesha
utawala wa kisheria.
Yahya Jammeh ambaye alishindwa na Adama Barrow katika uchaguzi wa
rais wa Gambia anapaswa kukabidhi madaraka ya nchi hii leo tarehe 19
Januari.
Wakati huo huo, mamia ya wananchi wa Gambia wameanza kuondoka nchini
humo wakikimbilia usalama wao katika nchi jirani. Thomas Cook, afisa wa
masuala ya utalii raia wa Uingereza amesema wameanza kuondoa watalii1000
hii leo huku wengine 2,500 wakitazamiwa kuondolea nchini humo hivi
karibuni.
No comments:
Post a Comment