Wednesday, January 25, 2017

WASOMALI 90 NA WAKENYA WAWILI WATIMULIWA MAREKANI

Raia takriban 90 wa Somalia na wawili wa Kenya wametimuliwa kutoka Marekani saa chache baada ya taarifa kuibuka kwamba Rais Donald Trump atakabiliana na watu wanaoishi nchini humo kinyume cha sheria.
Wote waliwasili katika uwanja wa kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi, lakini baadaye raia wa Somalia wakaendelea na safari hadi uwanja wa ndege wa Aden Abdulle mjini Mogadishu. Msemaji wa serikali ya Kenya Eric Kiraithe ameambia BBC kwamba ni kweli raia hao wamefukuzwa Marekani, ingawa hakusema iwapo hatua hiyo imetokana na msimamo wa Bw Trump.. "Ni watu 90 kulingana na habari ambazo tulipewa. Wakati unaondolewa nchi fulani kurejeshwa kwenu, huwa unarejeshwa hadi kwenu," ameambia BBC. Kuhusu sababu iliyowafanya kufurushwa, Bw Kiraithe amesema: "Inategemea sheria za nchi ambayo walikuwa wamehamia (Marekani),"

No comments:

Post a Comment