Watu waliokuwa na silaha wameivamia jela ya
Jau nchini Bahrain na kumuua polisi mmoja na kuwatorosha wafungwa wa
jela hiyo. Hayo yameelezwa na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Bahrain.
Shambulio hilo
limefanywa leo na watu wenye silaha katika jela ya Jau ambako
wanaharakati, wapinzani na raia waliokuwa wakiandamana dhidi ya serikali
ya Manama walikuwa wamefungwa. Jela hiyo yenye sifa mbaya inapatikana
kusini mwa mji mkuu wa Bahrain, Manama.
Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi hiyo imethibitisha katika taarifa
hii leo kuwa, watu wenye silaha walioivamia jela hiyo wamemuua kwa
kumpiga risasi askari polisi aliyetambulika kwa jina la Abdul Salam Saif
na kusababisha wafungwa kadhaa kutoroka. Taarifa ya Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Bahrain imeongeza kuwa jeshi tayari limeanza kuwasaka watu
waliohusika na shambulio katika jela ya Jau huko Manama pamoja na
wafungwa waliotoroka. Itafahamika kuwa maelfu ya wanaharakati wamefungwa
jela huko Bahrain kwa tuhuma mbalimbali kuanzia kushiriki katika
maandamano dhidi ya utawala wa Aal Khalifa na kuvishambulia vikosi vya
jeshi la nchi hiyo.
No comments:
Post a Comment