Wamarekani waliowengi wana shaka kuhusu uwezo wa rais mteule wa nchi hiyo wa kutekeleza majukumu yake.
Matokeo ya uchunguzi wa maoni uliofanywa na taasisi ya Gallup
yanaonesha kuwa, zaidi ya nusu ya Wamarekani wanaamini kwamba rais
mteule wa nchi hiyo, Donald Trump hawezi kusimamia migogoro mbalimbali
ya kimataifa.
Matokeo ya uchunguzi wa Gallup yanasema kuwa, asilimia 53 ya
Wamarekani wanaamini kuwa, Trump hataweza kutumia jeshi la Marekani kwa
njia za kimantiki.
Trump
Matokeo hayo yanaoana na yale yaliyofanywa awali na taasisi hiyohiyo
ya uchunguzi wa maoni ambayo yalionesha kuwa, kwa ujumla Doland Trump
ana umashuhuri na uungaji mkono mdogo zaidi akilinganishwa na marais
waliotangulia wa Marekani.
Matokeo ya uchunguzi huo uliofanywa baina ya tarehe 7 hadi 11 Disemba yalichapishwa jana katika mtandao wa Gallup.
No comments:
Post a Comment