Msemaji wa Wizara ya Ulinzi ya Russia amesema kuwa muungano unaoongozwa na Marekani unabomoa kwa makusudi miundombinu ya Syria.
Igor Konashenkov ametoa taarifa
Jumatano hii akieleza kuwa, muungano unaofanya mashambulizi dhidi ya
Daesh chini ya uongozi wa Marekani kuanzia mwaka 2012 hadi sasa
haujazishambulia ngome za kundi hilo, bali umebomoa na kuharibu kwa
makusudi miundombinu ya Syria.
Konashenkov ameongeza kuwa John Brennan
Mkuu wa Shirika la Kijasusi la Marekani (CIA) anafahamu vyema ukweli
huo; hii ni kwa sababu muda mrefu kabla ya kuanza oparesheni za kijeshi
za Russia huko Syria, muungano huo unaoongozwa na Marekani ulibomoa
miundombinu ya Syra kwa lengo la kuidhoofisha serikali halali ya nchi
hiyo.
Wizara ya Ulinzi ya Russia ilitoa
taarifa hiyo jana Jumatano kufuatia tuhuma zilizoelekezwa kwa Russia na
mkuu wa CIA aliyesema kwamba Moscow inatekeleza siasa za kuangamiza mali
na maliasili nchini Syria.
Msemaji wa Wizara ya Ulinzi ya Russia
amebainisha kuwa, mashambulizi ya anga ya nchi hiyo huko Syria yameua
maelfu ya magaidi; wakiwemo makamanda 204 wa magaidi hao katika medani
za vita.
Itakumbukwa kuwa Russia ilianzisha
mashambulizi ya anga huko Syria mwezi Septemba mwaka jana kufuatia ombi
la Rais wa nchi hiyo Bashar al Assad.
No comments:
Post a Comment