Katika
hotuba yake, Donald Trump (Pichani) ameahadi, kama katika kampeni yake ya uchaguzi
"kuifanya Marekani kuwa ni nchi yenye nguvu zaidi. "
Donald
Trump ameapishwa Jana Ijumaa, Januari 20 akiwa rais 45 wa Marekani katika
sherehe iliofanyika katika majengo makuu ya Bunge la Congress, Capitol
Hill saa 05:46 saa za Washington (sawa na saa 01:46 jioni saa za Afrika
ya Mashariki).
Baada ya
kufyatua mizinga 21 hewani, Donald Trump alitoa hotuba yake ya kwanza
kama rais. Donald Trump ameahadi kuwapa nafasi kubwa wananchi wa
Marekani katika madaraka, akisema kuwa wamewasahau kwa muda mrefu sana.
"Siku hii ya leo ni yenu na Marekani ni nchi yenu," amesema Obama.
Akiweka
mkono wake wa kushoto juu ya Biblia mbili, huku akiinua mkono wake wa
kulia, Donald Trump amekula kiapo mbele ya Rais wa Mahakama Kuu John G.
Roberts Jr. Na kuwa rasmi rais wa 45 wa Marekani.
Donald Trump ametoa kanuni mbili ambazo zitaongoza sera yake ya siasa "kununua vifaa vya Marekani, kuajiri Mmarekani."
Katika
hotuba yake, Donald Trump amesema anajutia kuona Marekani ilitajirisha
nchi za nje kwa gharama za Marekani. "Hayo yameshapita," Trump amesema.
"Tangu siku hii ya leo, Marekani itapewa kipaumbele sawa na suala la biashara, viwanda, au uhamiaji", amebaini Bw Trump.
"Tangu siku hii ya leo, Marekani itapewa kipaumbele sawa na suala la biashara, viwanda, au uhamiaji", amebaini Bw Trump.
Donald
Trump amehadi kuimarisha ushirikiano wa zamani na kujenga ushirikiano
mpya. "Ugaidi wa Waislamu wenye msimamo mkali utatokomezwa," Bw Trump
Ameonya.
Donald
Trump, alimaliza hotuba yake kwa maneno haya: "Tutaifanya Marekani kuwa
na nguvu zaidi, tutaifanya Marekani kuwa nchi tajiri zaidi, tutaifanya
Marekani kurudi kuwa na sifa zake, tutaifanya Marekani kurudi kuwa na
usalama wake. Kuifanya upya Marekani kuwa na nguvu “Make America great
again”. Hii ilikuwa kauli mbiu ya kampeni yake.
Kabla ya
kuapishwa kwa Donald Trump, Jaji wa Mahakama Kuu Clarence Thomas
amemuapisha Mike Pence, mgombea mwenza wa Donald Trump, ambaye amekua
rasmi makamu wa rais wa Marekani baada ya kuapishwa kwake.
Jackie Evancho, kijana wa miaka 16, amehitimisha sherehe hizo kwa kuimba wimbo wa taifa la Marekani.
Trump
amechukua hatamu kutoka kwa Rais Barack Obama saa mbili usiku Afrika
Mashariki. Amekula kiapo muda mfupi kabla ya saa mbili saa za
Washington.
No comments:
Post a Comment