Rais Enrique Pena Nieto wa Mexico kushoto na mwenzake wa Marekani Donald Trump kulia
Mexico
imesema kuwa haitalipia ukuta uliopendekezwa na rais wa Marekani Donald
Trump ,kulingana na rais wa taifa hilo Enrique Pena Nieto ambaye
ameshutumu mpango huo wa kujenga ukuta.
Hata
hivyo rais huyo hakizungumzia kuhusu iwapo atafutilia mbali ziara yake
ya Marekani ambapo anatarajiwa kukutana na rais Donald Trump.
Trump
tayari amesaini agizo la urais la kujenga ukuta kati ya Marekani na
Mexico na amesisitiza kuwa Mexico itailipa Marekani kwa ukuta huo.
Rais Pena Nieto aliambia taifa katika hotuba ya runinga kwamba :Nimesema tena na tena kwamba Mexico haitalipia ukuta huo.
''Ninajuta
na kushutumu uamuzi huo wa marekani wa kutaka kuendelea kujenga ukuta
ambao umetugawanya kwa miaka badala ya kutuunganisha''.
Lakini
Nieto amesema kuwa urafiki kati ya Mexico na raia wa Marekani utadumu
mbali na kutafuta suluhu kuhusu tatizo la wahamiaji.
Waziri wa
maswala ya kigeni nchini Mexico Luis Videgaray ambaye yuko mjini
Washington amesema kuwa rais huyo bado anaendelea kupima uwezekano wa
ziara ya Marekani siku ya Jumanne lakini akaongezea kuwa mkutano huo
bado utafanyika kufikia sasa.
No comments:
Post a Comment