Mkuu wa Shirika la Hija na Ziara la Jamhuri
ya Kiislamu ya Iran amekanusha madai ya Saudi Arabia kuwa imetuma barua
ya mwaliko kwa Iran wa kushiriki kwenye Hija ya mwaka ujao.
Siku
ya Alkhamisi iliyopita, Waziri wa Hija na Umra wa Saudi Arabia,
Muhammad Benten alitangaza kuwa Riyadh imetoa mwaliko kwa ujumbe wa
Shirika la Hija na Ziara wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran wa kuhudhuria
kikao cha kuratibu maandalizi ya Hija.
Hamid
Muhammadi, Mkuu wa Shirika linaloshughulikia masuala ya Hija na Ziara la
Iran amevieleza vyombo vya habari kuwa hakuna barua ya mwaliko
iliyotumwa na Saudia kwa ajili ya Hija ya mwaka ujao na kusisitiza
kwamba Shirika la Hija na Ziara na Ofisi ya Kiongozi Muadhamu ya Masuala
ya Hija zinafuatilia kwa uwezo wao wote kuondolewa vizuizi vya Hija.
Muhammadi
ameongeza kuwa kuvunjwa uhusiano wa kisiasa kati ya Iran na Saudia
kumesababisha kufungwa ubalozi wa Iran mjini Riyadh na balozi zake ndogo
zilizoko mjini Jeddah na kwamba ikiwa serikali ya Saudi Arabia
itatekeleza masharti yanayodhamini izza, usalama na heshima ya mahujaji
na wafanya ziara wa Iran, Jamhuri ya Kiislamu itashiriki katika Hija
ijayo.
Itakumbukwa kuwa kutokana na usimamizi mbovu wa utawala wa Aal Saud
katika Hija ya mwaka jana, zaidi ya mahujaji elfu saba wakiwemo mahujaji
477 kutoka Iran walifariki dunia katika maafa mawili yaliyotokea kwenye
msikiti mtukufu wa Makka na eneo la Mina.
Kwa
kutumia kisingizio cha madai yasiyo na msingi, serikali ya Saudia mwaka
huu iliwazuilia njia ya kutekeleza ibada tukufu ya Hija wafanya ziara wa
baadhi ya nchi za Kiislamu ikiwemo Iran na Syria…/
No comments:
Post a Comment