Jeshi la Yemen Jumatatu ya jana liliangamiza
meli ya mizinga ya Saudia na kusababisha makumi ya askari wa nchi hiyo
vamizi kuangamizwa na wengine kujeruhiwa.
Sambamba na Saudia kukiri juu ya habari hiyo imedai kuwa,
katika shambulizi la jeshi la Yemen dhidi ya meli yake ya mizinga katika
pwani ya mkoa wa Al Hudaydah, askari wake wawili waliuawa na wengine
watatu kujeruhiwa. Wakati huo huo jeshi la Saudia limeshambulia mji
mdogo wa pwani wa Al Mukha kusini mwa mkoa wa Taiz na kusababisha makumi
ya raia kuuawa shahidi na wengine wengi kujeruhiwa.
Aidha shambulizi hilo lilililenga daraja la Irfan mjini
humo. Kwingineko jeshi la Yemen kwa kushirikiana na harakati ya wananchi
ya Answarullah imeangamiza askari vibaraka wa Saudia waliokuwa
wanakimbia uwanja wa mapigano baada ya kuzidiwa. Kwa mujibu wa habari
hiyo askari kadhaa vibaraka wa Aal-Saud wameangamizwa katika mkoa wa
Taiz kusini magharibi mwa Yemen.
Hii ni katika hali ambayo kwa mara nyingine jeshi la Yemen
limezilenga kambi za jeshi la Saudia za Jizan na kuisababisha nchi hiyo
kibaraka wa Marekani na Israel hasara ya maafa na uharibifu. Kama
ambavyo jeshi hilo la Yemen na harakati ya Answarullah limeshambulia kwa
makombora mengi kambi ya jeshi ya al-Makhruq iliyopo eneo la Quwah
mkoani Najran na kuangamiza askari kadhaa.
No comments:
Post a Comment