Rais
Barack Obama ametoa hotuba yake ya mwisho akiwa kama rais wa Marekani,
huko Chicago hotuba ambayo ilijaa hisia kali na kupelekea kutokwa na
machozi yeye pamoja na baadhi ya watu.
Rais
wa Marekani Barack Obama amewahimiza Wamarekani kuitetea demokrasia,
kwenye hotuba yake ya mwisho kama rais wa Marekani mjini Chicago.
"Kwa
kila kipimo, Marekani sasa ni bora zaidi, na ina nguvu zaidi" kuliko
ilivyokuwa miaka minane iliyopita alipochukua madaraka, amewaambia
maelfu ya wafuasi wake waliokusanyika mjini humo.
Hata hivyo, "demokrasia inatishiwa kila inapokosa kutiliwa maanani".
Amewaomba
Wamarekani wa kila asili kuangazia mambo kutoka kwa msimamo wa wengine,
na kusema kwamba "lazima tuwategee sikio wengine na kusikia".
Rais
Obama ndiye rais wa kwanza nchini Marekani wa asili ya Afrika na
alichaguliwa mwaka 2008 akiahidi kurejesha matumaini na kutekeleza
mabadiliko.
Mrithi wake Donald Trump ameahidi kubatilisha baadhi ya sera kuu alizofanikisha Bw Obama, 55.
Michelle
Obama akimliwaza binti yake Milia ambaye alijikuta akitokwa na machozi
wakati akisikiliza hotuba ya baba yake Rais Barack Obama
Makamu wa rais wa Marekani Joe Biden naye alijikuta akishindwa kujizuia na kutokwa na machozi
Rais wa Marekani, Barack Obama akikumbatiana na Makamu wa rais wa Marekani Joe Biden baada ya kumaliza hotuba yake.
Michelle Obama akimkumbatia mumewe rais Barack Obama baada ya kumaliza hotuba yake.
Rais wa Marekani Barack Obama akimkumbatia binti yake Milia baada ya kumaliza hotuba yake.
No comments:
Post a Comment