Maafisa wa usalama Gambia wamefunga vituo
viwili vya radio binafsi karibu na mji mkuu Banjul huku nchi hiyo
ikikumbwa na mgogoro wa baada ya uchaguzi.
Jumuiya
ya Waandishi wa Habari wa Gambia ilisema jana kuwa, vituo vya redio vya
Teranga FM na Hilltop Radio vilifungwa juzi Jumapili katika oparesheni
iliyoendeshwa na maafisa wa polisi na maafisa wa usalama wa taifa.
Serikali haijatoa taarifa yoyote kuhuhsiana na tukio hilo.
Mgogoro
wa kisiasa Gambia uliibuka pale Rais Yahya Jammeh ambaye kipindi chake
cha kuweko madarakani kinamalizika tarehe 19 ya mwezi huu wa Januari,
alipokataa matokeo ya uchaguzi ingawa awali alikuwa amekubali kushindwa,
na hivyo kuzusha hofu ya uwezekano wa mataifa ya eneo la magharibi mwa
Afrika kuingilia kati na kumuondoa madarakani kwa nguvu.
Katika hotuba yake hiyo ya mwaka mpya
Rais wa Gambia amesema, azimio lililopitishwa na ECOWAS kwamba itatumia
kila njia iwezekanayo kuhakikisha matokeo ya uchaguzi wa rais wa Gambia
yanaheshimiwa, ni kutangaza vita na kuivunjia heshima katiba ya nchi
hiyo.
Jammeh
ametangaza kuwa hatokabidhi madaraka; lakini rais mteule wa nchi hiyo
Adama Barrow ametoa wito tena kwa kiongozi huyo kumtaka angátuke
madarakani kwa njia za amani.
No comments:
Post a Comment